Waokoaji wakishika miguu ya Fi asijirushe ghorofani jini Zhanjiang, China
SHENG FI, ni mwanamke anayeishi katika mji wa Zhanjiang, kusini mwa China. Hivi majuzi, alimwua mtoto (mpwaye) wa wifi yake mwenye umri wa miaka minne na kumtupa kutoka chini kutoka juu ya jengo la ghorofa nne. Hii ni baada ya ugomvi na wifi yake huyo.
Baada ya hapo Fin aye alitaka kujirusha kwenda chini, lakini aliokolewa na wafanyakazi wa jengo hilo ambao walipanga njama za kumzuia kujirusha chini kwa kumwita binti yake aliyekuja kumlaghai kwa maneno kabla hawajamkamata.
Kwa mujibu wa polisi, kwa kitendo hicho, mwanamke huyo atauawa kwa kupigwa risasi baada ya yeye kukiri kumwua mtoto huyo.
Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, China inashika nafasi ya tisa duniani kwa watu kujiua ambapo wahusika wakuu wa ‘mauaji’ haya makubwa kuliko yote nchini humo ni watu kati ya miaka 15 hadi 34.
Miongoni mwa nchi zinazoongoza duniani kwa kujiua ni Latvia, Kazhakstan na Korea ya Kusini.
Binti wa Fi ( wa pili kulia) aliyefika kumlaghai Fi asijiue. Binti huyo alikuwa hajui mama yake alikuwa amemwua mpwaye.
Fi akikokotwa kupelekwa kwenye usalama.
No comments:
Post a Comment