Wednesday, August 29, 2012

MISS MWANZA 2012 NI MTIKISIKO IJUMAA



FAINALI za Miss Mwanza 2012, zinatarajiwa kulitikisa Jiji la Mwanza Ijumaa hii.
Shindano hilo mwaka huu, limeonesha kuwa na msisimko wa hali ya juu kutokana na hali halisi kujionesha kwamba warembo
wa shindano hilo mwaka huu ni tishio hata kwa Miss Tanzania.
Tathmini ya mashindano ngazi mbalimbali kuelekea Miss Tanzania mwaka huu, inaonesha kuwa mrembo atakayeshinda Miss
Mwanza mwaka huu, anayo nafasi kubwa ya kuchukua taji.
Wasichana hao wazuri, wanaostahili sifa ya kuitwa warembo, ndiyo watakaopanda jukwaani kesho (Agosti 31, 2012) kwenye
Ukumbi wa Yacht Club, Mwanza, kuwania la Taji la Miss Mwanza 2012.
Warembo hao, tayari wapo kambini ndani ya Isamilo Lodge, wakijiandaa na mtifuano mkali.
Mratibu wa shindano hilo, Peter Omar, amesema: “Kila kitu kipo sawa, maandalizi ni mazuri. Kusema ukweli kambi ya Miss
Mwanza mwaka huu ni matawi ya juu. Warembo wapo vizuri na huduma pia ni za kiwango kizuri. Kimsingi kambi ya mwaka huu imepandisha hadhi ya shindano letu.”
Kwa upande mwingine, Omar alisema, wakongwe wa Taarab nchini, Malkia Khadija Kopa na gwiji Mwanahawa Ali, wanarajiwa
kuoneshana mkali wa vijembe vya mwambao kwenye shindano la Miss Mwanza 2012-2013.
Kopa na Mwanahawa ambao ndiyo waimbaji wakongwe walio juu kwa sasa kwenye muziki wa Taarab, wanarajiwa kutoa shoo
kali siku hiyo kisha mashabiki wenyewe ndiyo watapima nani mkali wa mipasho.
“Miss Mwanza ya mwaka huu ni funga kazi. Watakaokuja Yacht Club, watashuhudia shoo kali ambayo haijawahi kutokea.
Kwanza kabisa tuna warembo wazuri. Hii ina maana kwamba Miss Tanzania wa mwaka huu, atatokea Mwanza.
“Tuna timu nzuri ya wanamuziki watakaotumbuiza. Mpambano wa Khadija Kopa na Mwanahawa Ali, haujawahi kutokea
Mwanza. Kuna wanamuziki wengine wakali watakuwepo akiwemo Bob Haisa (Haisa Mbyula) ambaye kwa zaidi ya miaka 14,
amebaki kuwa mmoja wa mabalozi bora kabisa wa Kanda ya Ziwa kwa upande wa muziki wa kizazi kipya.”



Warembo Redds Miss Mwanza 2012/13 wakiwa kambini katika Hoteli ya Isamilo Lodge, ambapo warembo 18 kutoka wilaya zote za Mkoa wa Mwanza, watashiriki shindano hilo, linalotarajiwa kufanyika siku ya Ijumaa tarehe 31/08/2012 ndani ya Yatch Club jijini Mwanza.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...