Thursday, August 2, 2012

MISS MWANZA 2012 KUFANYIKA AGOSTI 31 MWAKA HUU



  SHINDANO la kumpata mrembo wa mkoa wa Mwanza 2012/13 linatarajiwa kurindima Ijumaa ya Agosti 31 mwka huu ndani ya Ukumbi wa Yatch Club jijini Mwanza.
Kwamujibu wa taarifa iliyotolewa na muaandaji wa kampuni ya Sisi Entertainment
John Doto, amesema shindano hilo linalovuta hisia za wengi ndani ya mkoa wa Mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla,
litashirikisha warembo tariban 20 kutoka wilaya zote za mkoa Mwanza.

John Doto amesema warembo wote watakaa kambini kwa wiki mbili, ambapo kambi rasmi itaanza
tarehe 20 agosti mwaka huu katika hoteli ya Isamilo Lodge.
Shindano
la Redds Miss Mwanza 2012/13, lilisogezwa mbele kufuatia mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Wakiwa kambini warembo watapata fursa ya kujifunza Mitembeo, Tabasamu, ufahamu wa
kujieleza pamoja na kuvumbua vipaji mbalimbali.

John Dotto pia amesema warembo watakua na ziara ya kwenda kwenye mbuga za wanyama Serengeti,
kutoa misaada kwa watoto yatima, vikongwe pamoja na kufanya usafi kwenye moja
ya Hospitali Jijini Mwanza na moja ya barabara za Mwanza.

Kwa miaka ya hivi karibuni, Mkoa wa Mwanza umekua ukitoa warembo wanaofanya vizuri
mashindano ya Taifa.

Itakumbukwa mwaka 2008 Nasreem Karim na Mwaka 2009 Miriam Gerald waliweza kushika Mataji ya Miss Tanzania wakitokea mkoa Mwanza.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...