Wednesday, August 22, 2012

MICHUANO YA AIRTEL RISING STARS YAANZA NAIROBI


Mkurugenzi wa Masoko wa Timu ya Manchester United,Jonathan Rigby (kulia) akikabidhi jezi kwa Waziri Mkuu wa Kenya,Mh. Raila Odinga (kushoto) wakati wa ufunguzi rasmi wa Mashindano ya Airtel Rising Stars kwa Afrika yatayofanyika jijini Nairobi,Kenya.Wengine pichani ni Manoj Kohli CEO (International) & Joint MD,Ofisa Mkuu wa Masoko wa Bharti Airtel na Airtel Africa,Andre Beyers (wa tatu kulia).

Michuano ya Airtel Rising Stars barani Afrika imeanza kutimua vumbi Jijini Nairobi, Kenya. Michuano hiyo imeleta pamoja wavulana na wasichana wenye umri chini ya miaka kumi na saba na itaendelea mpaka Agosti 25.


Michuano hiyo ambayo ilianzia kwenye ngazi ya wilaya mpaka Taifa na kufanyika kwenye nchi 15 barani Afrika. Huu ni mpango kabambe wa Airtel Rising Stars, wenye lengo la kuwapa vijana chipukizi fursa ya kuonyesha vipaji vyao. Ikiwa ni ya moja ya michuano mikubwa kabisa barani Afrika, jumla ya timu 18,000 zilishiriki na wachezaji 324,000 – wavulana na wasichana kushiriki. Hii ndio mara ya kwanza kushirikisha wasichana.


Michuano hiyo ilifunguliwa rasmi na Waziri Mkuu wa Kenya, Mh Raila Odinga – akisindikizwa na Mtendaji Mkuu wa Bharti Airtel Afrika – Manoj Kohli.


Michuano hiyo pia itaashiria uzinduzi wa kliniki mbili za soka za kimataifa zitakaozoendezwa na makocha kutoka klabu kubwa duniani – Arsenal na Manchester United – zote za Uingereza. 


Kwenye uzinduzi wa michuano hiyo pia walikuwepo wawakilishi kutoka kwenye Klabu hizo ambao ni Mkurugenzi wa Masoko kutoka Timu ya Manchester United,Jonathan Rigby na Mkurugenzi Masoko kutoka Arsenal Angus Kinnear. Uzinduzi wa kliniki utafanyika na wachezaji wa zamani wa Manchester United Peter Schmeichel na Ray Parlour kutoka Arsenal.


Kwenye mechi za ufunguzi, timu ya wasichana ya Kenya ilishushia kipigo cha magoli 11 wenzao wa Malawi wakati kwa upande wa wavulana Malawi ilishinda 5- dhidi ya Kenya.

Mkurugenzi wa Masoko wa Timu ya Arsenal,Angus Kinnear (kushoto) akimkabidhi jezi Waziri Mkuu wa Kenya,Mh. Raila Odinga wakati wa ufunguzi rasmi wa Mashindano ya Airtel Rising Stars yatayofanyika jijini Nairobi,Kenya.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...