Mbunge wa jimbo la Bumbuli Mhe. January Makamba akiongea na wakazi kutoka wilaya ya Lushoto jimbo la Bumbuli katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam leo mkutano huo ulikuwa unajadili maendeleo ya jimbo la Bumbuli na kutambulisha shirika la maendeleo la Bumbuli, January Makamba amesema katika kipindi cha mwaka 2011-2012 kiwango cha elimu ya wilaya hiyo imekuwa chini na kusababisha vijana wengi katika mkoa wa Tanga kuwa na sifa ya kuuza chipsi na kubeba mizigo badala ya kufanya kazi kwenye makampuni.
Mkurugenzi wa shirika la Bumbuli Bw. Najim Msenga (kushoto), mwenyekiti mteule wilaya ya Bumbuli Bw. Amiri Sheiza (kulia)katibu wa CCM wilaya ya Lushoto Bw. Loth Ole Lemeirut (katikati)wakijadiliana jambo mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo leo
Wakazi kutoka jimbo la bumbuli wakiwa katika mkutano huo wa kujadili maendeleo ya wilaya ya Bumbuli
Kikundi cha ngoma kijulikanacho Mount Usambara Voice kikitoa burudani katika mkutano huo
Katibu wa CCM wilaya ya Lushoto Bw. Loth Ole Lemeirut (kushoto)na mwanakamati wa shirika la Bumbuli Bw. Naaman Shauri wakifuatilia kwa umakini mada iliokuwa ikendelea katika mkutato huo leo
HABARI/PICHA:FULLSHANGWE BLO
No comments:
Post a Comment