Friday, August 17, 2012

KWAKUFANYA HAYA UTANOGESHA PENZI LAKO SIKU YA SIKUKUU YA IDD

 Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya Naseeb Abdul, akiwa kwenye hali ya malavidavi na Wema Abraham Isaac Sepetu.
 NI kweli kabisa kwamba, kwa wapenzi wanaopendana kwa dhati kila siku ni sikukuu kwao. Hata hivyo, sina budi kuwakumbushia baadhi ya mambo ambayo ni vyema mkafanyiana katika sikukuu hii ya Idd inayokuja, lengo likiwa ni lilelile la kulinogesha penzi lenu.
Jifungieni chumbani
Hili si kwa wale walio nje ya ndoa, nawazungumzia wale ambao wamehalalishwa kufanya mapenzi, nawazungumzia wanandoa na siyo nyie mnaodanganyana na kuvunja amri ya sita.Kwa wanandoa, yawezekana siku hiyo mkawa hamjisikii kutoka kwenda popote, basi tulieni chumbani kwenu. Cha kufanya siwezi kuwafundisha ila mahaba ya siku hiyo si vibaya yakawa tofauti na ya siku zote.Naelewa wengi mlikuwa mkipeana mambo kwa kujibanabana kutokana na kuwepo kwenye mwezi mtukufu. Tumieni siku hizo kumaliza kiu yenu.Kama chumbani kwenu mtakuwa mmepakinahi, tafuteni hoteli iliyotulia muende mkapumzike kwa raha zenu.
Kununuliana zawadi
Siku zote zawadi ni chachandu katika penzi. Kumbuka kwamba katika suala la uhusiano, zawadi ni zawadi bila kujali ukubwa wake. Hii itategemea tu na uwezo wako. Kwa maana hiyo basi ni vizuri ukamwandalia zawadi nzuri mwenza wako ambayo itamfanya aione siku hiyo ni muhimu kwenu.

Kadi maalum
Hili kwa wengine itakuwa ni kama kuwakumbushia. Usisahau kabisa kumwandalia mpenzi wako kadi ya kumtakia Idd njema.Urasmi katika hili ni wa kuzingatiwa, angalia kadi yenye rangi za kimahaba na ujumbe ulio muruwa.
Tokeni muende kokoteYawezekana katika kipindi chote cha uhusiano wenu hamjawahi hata siku moja kutoka pamoja kwenda kwenye ukumbi wa starehe ama sehemu yoyote tulivu. Kwa sikukuu hii inayokuja si vibaya ukafanya hivyo na kama mna utaratibu wa kufanya hivyo kila wikiendi, safari hii mnaweza kupanga kwenda sehemu tofauti ikiwezekana hata kutoka nje ya mji mnaoishi. Kuna mengi ya kufanya mnapotoka ‘out’, mojawapo ni kubadilishana mawazo juu ya maisha yenu, kuombana msamaha pale ambapo mlitokea kutofautiana. Yaani ni kipindi cha kulikarabati penzi lenu na hata pale mtakapokuwa mnarudi inakuwa ni kama vile mnafungua ukurasa mpya.

‘Surprise’
Surprise zipo za aina nyingi, kwa mfano inawezekana hujamuambia mpenzi wako chochote kuhusu sikukuu lakini siku hiyo unaweza kumshitukiza kwa zawadi, kumvisha pete ya uchumba, kumtoa ‘out’ na mambo mengine ambayo yatamfurahisha utakopomfanyia kwa kum-surprise.

Ni siku za furaha
Ninachotaka kusisitiza hapa ni kwamba, hakuna kitu kibaya kama wapenzi katika siku hizi kununiana ama kuudhiana. Hizi ni siku za furaha hivyo basi, hakikisha unafanya kila uwezalo kumfanya mwenza wako awe na uso wa tabasamu muda wote.Jamani ni hayo tu, niwatakie sikukuu njema.




No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...