Saturday, August 4, 2012

KIDUMU:KUMBE CHAELEONE, WAKALA DILI LAO MOJA TU


Joseph Mayanja ‘Chameleone

 
kidum

Kuna hoja nyingi zimeibuka. Wapo watu ambao wamejaribu kupotosha ukweli kwa makusudi kuhusu sakata la msanii tapeli wa Uganda, Joseph Mayanja ‘Chameleone’, alivyoitapeli Kampuni ya Global Publishers and General Enterprises Ltd.

Msimamo wa Global upo wazi kuwa Chameleone alicheza faulo, lengo lake likiwa kujipatia fedha zaidi baada ya kuona kwamba anahitajika mno kuja Tanzania kufanya shoo ya Usiku wa Matumaini, iliyofanyika Julai 7, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.…
 
Joseph Mayanja ‘Chameleone
Kuna hoja nyingi zimeibuka. Wapo watu ambao wamejaribu kupotosha ukweli kwa makusudi kuhusu sakata la msanii tapeli wa Uganda, Joseph Mayanja ‘Chameleone’, alivyoitapeli Kampuni ya Global Publishers and General Enterprises Ltd.
Msimamo wa Global upo wazi kuwa Chameleone alicheza faulo, lengo lake likiwa kujipatia fedha zaidi baada ya kuona kwamba anahitajika mno kuja Tanzania kufanya shoo ya Usiku wa Matumaini, iliyofanyika Julai 7, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Tumeshafafanua kuwa mwanamuziki huyo hakunyang’anywa passports ila alikimbia hotelini (The Atriums Hotel) wakati alipotakiwa kulipa fedha alizotapeli ambazo ni Dola za Kimarekani 3,500.
Inawezekana Chameleone na wenzake, walikuwa wanakimbilia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ili watoroke na ndege bila kulipa fedha lakini wakaja kugundua kwamba passports waliziacha hotelini.
Hapo wakaanza kueneza propaganda za maneno kuwa walinyang’anywa passports zao. Walieneza maneno hayo, wakitambua fika kwamba wanasema uongo usiomithilika. Wamepata dhambi nyingi kwa uongo wao.
UKWELI WA PASSPORT
Ni kawaida ya Hoteli ya The Atrium, kutunza fedha na nyaraka nyingine muhimu za kila mgeni anayeingia kwenye hoteli hiyo. Vitu hivyo huhifadhiwa ili isitokee mgeni kudai ameibiwa nyaraka zake muhimu au fedha.
Hivyo basi, Chameleone na wenzake wawili, mmoja DJ wake, mwingine msindikiza sauti wake (back vocalist), walikabidhi hati zao kusafiria mapokezi kwenye hoteli hiyo, siku ya kwanza walipofika.
Inawezekana wakati akina Chameleone wanatoroka pale hotelini, walijisahau kama passports zao wameziacha mapokezi. Baadaye walipogundua wameziacha, wakaona hawana kitu cha kufanya zaidi ya kudai wamenyang’anywa, lengo likiwa kutafuta huruma kwa jamii.
KUNA MASWALI YA KUJIULIZA
Mosi: Baada ya kudai passports amenyang’anywa, ilikuaje tena Chameleone akavuka mpaka Uganda?
Pili: Bila shaka alitumia njia za panya, je, ni nani aliyemsaidia au ni asili ya uhuni wake?
Tatu: Je, hatuoni kama Chameleone ameonesha dharau kwamba mipaka ya nchi yetu inaweza kuvukwa bila passport?
Nne: Kama kweli alinyang’anywa passport, ni kwa nini hakufungua mashitaka hapa nchini, badala yake akakimbilia Uganda kwenda kufanya fujo kwenye ubalozi wa nchi yetu?
Tano: Je, Chameleone anadharau Watanzania na jeshi lao kiasi kwamba hakutaka kupeleka madai yake polisi?
Mwisho wa kujiuliza maswali hayo, bila shaka utapata jawabu kwamba msanii huyo ni muongo, tapeli wa kutupwa, aliyeamua kudanganya amenyang’anywa passport kwa lengo la kuuzuga umma.
UKWELI WA KIDUM
Kidum (Jeane Pierre Nimbona), Jumatano iliyopita alizungumza kwenye Kipindi cha Amplifier, Radio Clouds FM, akielezea jinsi alivyokwenda Uganda na kujiridhisha ukweli kwamba Chameleone na wakala, George Mugabo, wanafahamiana na kama kweli, wamezungumza kuhusu ‘dili’ la msanii huyo Mganda kuja Tanzania Julai 7.
Kwa mujibu wa Kidum, kama alivyosikika kwenye kipindi hicho, ni kweli alikwenda Kampala, Uganda kama alivyoombwa na Global ili kupata uthibitisho na akiwa huko, alijiridhisha kuhusu mazungumzo ya George na Chameleone kisha akasimamia malipo kufanyika.
Hapa utaona kwamba Global ni watu wenye akili timamu, ndiyo maana hawakutaka kwenda kichwakichwa. Walitaka kujirisha kuhusu uhalali wa George kupewa fedha kwa niaba ya Chameleone na kweli Kidum, alijiridhisha ndiyo maana malipo yalifanyika.
Kidum pia alieleza kwamba akiwa Uholanzi, alimpigia simu Chameleone kumuulizia kuhusu maendeleo ya shoo ya Julai 7, msanii huyo wa Uganda akadai hajapewa fedha na George.
Hata hivyo, baada ya muda mfupi Chameleone alimtumia SMS Kidum, akamwambia ampigie muda huo, kwamba yupo na George.
Kweli Kidum akapiga halafu Chameleone akawa anatoa sauti: “Nipe pesa ulizopewa na Kidum.” Mtu ambaye alisema ni George akawa anasikika kwenye simu anasema: “Samahani, pesa nimetumia.” Halafu Chameleone akasema: “Unaona Kidum, huyu mtu kala hela zenu, mimi nikipata hizo pesa nitaenda Tanzania kufanya hiyo shoo.”
Ifahamike kuwa Chameleone kwenye nukuu zake, amekuwa akidai hamfahamu George, sasa jiulize maswali haya;
Mosi: Ilikuaje alipopigiwa simu na Kidum, Chameleone alimpata George ndani ya muda mfupi na kudai yupo naye?
Pili: Kama kweli hamjui, ilikuaje wakazungumza kwa simu kisha akatoa sauti ya kumruhusu akamilishe dili?
Majibu ya maswali hayo, yanazidi kuonesha kwamba Chameleone na George, lao moja. Walicheza dili kuizunguka Global na Kidum, sasa baada ya mambo kuwa magumu, ikabidi mwanamuziki huyo amkane wakala wake.
Hivi karibuni, Kidum alikuwepo Uganda na akaonana na George. Baada ya kukutana, Kidum alikumbushia madai ya dola 3,500 ambazo alizipokea na kumpa Chameleone.
Hata hivyo, George badala ya kujibu wanalipaje fedha, alianza kutoa malalamiko dhidi ya Chameleone kwamba alimuwezesha kupata dola 8,000, lakini hakumlipa chochote.
Kwamba, katika zile dola 8,000 ambazo Global ilimlipa Chameleone mara ya pili, George anadai hakupata mgao. (Hivyo ndivyo alivyomlalamikia Chameleone).
Kauli hiyo inamaanisha kuwa George na Chameleone, wamekuwa na mchezo wa kutapeli na kugawana fedha, ndiyo maana wakala huyo akamlalamikia Kidum, kwamba hakupata mgao kwenye fedha za mara ya pili.
Maelezo hayo, ukijumlisha na asili ya Chameleone kuchukua fedha za mapromota kisha kuingia mitini (mfano mmojawapo ni namna alivyomtapeli John Dilinga ‘DJ JD’), unaona wazi namna msanii huyo alivyoitapeli Global.
USIKOSE KUSOMA GAZETI LA IJUMAA WIKIENDA JUMATATU, LITAKAPOFUNGA MJADALA HUU.


No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...