Friday, August 3, 2012

HABARI NJEMA KWA WASOMAJI WA MAGAZETI PENDWA, JISHINDIE NOAH KWA KUSOMA MAGAZITI...




Na Mwandishi Wetu

KUPITIA magazeti ya Global Publishers, likiwemo hili la Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Uwazi, Amani, Risasi na Championi, sasa msomaji wake atatimiza ndoto yake ya kumiliki gari kwani ataiweka mikononi gari aina ya Toyota Noah.

Akizungumzia promosheni hiyo kubwa inayokwenda kwa jina la Timiza Ndoto Yako, Miliki Noah, Meneja wa Global Publishers, Abdallah Mrisho alisema kuwa mbali na gari hilo, wasomaji watajishindia vitu vingine vya thamani zikiwemo runinga za kisasa yaani flat screen na simu kali za BlackBerry.
Mrisho alisema kuwa mbali na wasomaji pia mawakala watapata fursa ya kujishindia mtaji taslimu wa Sh. milioni moja huku ‘mavenda’ wakijinyakulia baiskeli.
“Ni fursa nyingine kwa wasomaji wa magazeti ya Global kutimiza ndoto zao kwa kumiliki gari na vitu vingine vya thamani. Promosheni itachukua miezi mitatu na itaanza Agosti 10, mwaka huu. Msomaji anachotakiwa kufanya ni kusoma magazeti yetu kwa wingi kila siku ili kujinufaisha,” alisema Mrisho.
Ni desturi ya Global Publishers kuwanufaisha wasomaji wake kwa kuwasaidia kutatua changamoto za kimaisha ambapo huko nyuma ilishatoa magari ya thamani kubwa na zawadi nyingine kibao. Kwa habari zaidi, soma magazeti ya Global.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...