Thursday, August 9, 2012

BENKI YA KIISLAM YA WATU WA ZANZIBAR PBZ JANA WALIPO FUTURU NA MAKAMU WA RAIS DKT BILAL



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongazana na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Juma Amour, wakati alipowasili kwenye ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam jana, kuhudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki hiyo na kufutari pamoja na baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislamu walioalikwa.

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kulia) akiwaongoza baadhi ya Viongozi wa dini na Serikali ‘kujisevia’ futari wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) na kufuturu pamoja na Makamu wa Rais Dkt. Bilal na baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislamu walioalikwa katika hafla hiyo, jana.

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kulia) akiwaongoza baadhi ya Viongozi wa dini na Serikali ‘kujisevia’ futari wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) na kufuturu pamoja na Makamu wa Rais Dkt. Bilal na baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislamu walioalikwa katika hafla hiyo, jana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Juma Amour, akizungumza machache kuhusu kazi na utendaji wa kazi za Benki hiyo ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) na malengo yake wakati wa hafla hiyo ya futari iliyofanyika jana katika Ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Akitoa neno la shukrani kwa mgeni rasmi Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo.

Baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislam waliohudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) wakipata futari wakati wa hafla hiyo.

Baadhi ya Waumini wa dini ya Kiislam waliohudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) wakishiriki kuomba dua ya pamoja wakati wa hafla hiyo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, na baadhi ya waumini wa dini ya kiislam baada ya hafla hiyo ya futari iliyoandaiwa na Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) jana katika ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Sheikh, Abdulla Tarib Abdulla na baadhi ya waumini wa dini ya kiislam baada ya hafla hiyo ya futari iliyoandaiwa na Benki ya Kiislam ya Watu wa Zanzibar (PBZ) jana katika ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...