Tuesday, July 24, 2012

WAZIRI WA MIUNDOBINU NA MAWASILIANO Z'BAR AJIUZULU


Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar aliyeziuzulu, Hamad Masoud Hamad.
Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano wa Zanzibar, Mh. Hamad Masoud, amejiuzulu kutoka katika nafasi hiyo kufuatia ajali ya Meli ya MV Skagit iliyotokea mwishoni mwa wiki iliyopita.

Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Insp. Mohamed Mhina amesema kuwa nafasi ya Waziri imechukuliwa na Mwakilishi wa Jimbo la Ziwani Kusini Pemba Mh. Rashid Seif Sulein. Mheshimiwa Hamad yeye alikuwa ni mwakilishi wa Jimbo la Ole Kaskazini Pemba. Waziri Hamad amechukua uamuzi huo kama sehemu ya kuonyesha uwajibikaji mbele ya umma na kuonyesha mfano kwa viongozi wengine. Kabla ya kujiuzulu, waziri Hamad alimwandikia barua Rais wa Zanzibar Ali Mohammed Shein kumwelezea hatua hiyo na kuomba amruhusu kujiuzulu hatua ambayo Rais ameikubali na kumteua mbadala yake.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...