MISS USTAWI 2012 HUYU HAPA
Miss Ustawi wa Jamii 2012, Hilda Edward (katikati) akiwapungia mikono mashabiki wake baada ya kutwaa taji hilo sambamba na mshindi wa pili Nancy Maganga (kushoto) na mshindi wa tatu, Ndenisia Mbowe.
MISS Ustawi wa Jamii usiku wa kuamkia leo ilifana vilivyo ndani ya
Ukumbi wa New Maisha Club, ambapo Hilda Edward alifanikiwa kuibuka na
taji hilo huku Nancy Maganga akimfuatia kwenye nafasi ya pili na
Ndenisia Mbowe alichukua nafasi ya tatu.
Mshindi wa kwanza alizawadia kompyuta mpakato ‘laptop’, mshindi wa pili alipewa shilingi 300,000 na mshindi wa tatu 200,000 huku mshindi wa nne akiambulia kifuta jasho cha shilingi 100,000. Washiriki waliobakia walipewa kifuta jasho cha shilingi 40,000 kila mmoja.
Baadhi ya washiriki waliofanikiwa kutinga hatua ya tano bora wakiwa katika pozi la pamoja.
Mshindi wa kwanza alizawadia kompyuta mpakato ‘laptop’, mshindi wa pili alipewa shilingi 300,000 na mshindi wa tatu 200,000 huku mshindi wa nne akiambulia kifuta jasho cha shilingi 100,000. Washiriki waliobakia walipewa kifuta jasho cha shilingi 40,000 kila mmoja.
Baadhi ya mashabiki wakiserebuka wakati wa makamuzi hayo ndani ya ukumbi huo.
No comments:
Post a Comment