WAFANYAKAZI WA AIRTEL NA WATEJA WAO WAJUMUIKA QUALITY CENTRE DAR
Huu ni mkakati ambao Airtel imejiwekea kusherehekea pamoja na watoto wa wateja wao wa makapuni ( corporate customer) wiki moja kabla ya sikukuu za Pasaka lengo likiwa ni kuwa karibu na wateja wao na
kusambaza upendo wa kampuni hiyo kwa wateja wake na familia zao.
Akiongea kwa niaba ya Airtel Mkurugenzi wa Biashara wa Airtel Bi Irene Madege alisema: "Leo tunajisikia furaha kuwa na watoto wa wateja wetu na kujumuika nao pamoja, tumekuwa tukifanya shughuli mbalimbali ikiwa ni katika kuwazawadia wateja wetu, lakini leo tunatumia muda huu kuwapa burudani watoto ambao ndio wateja wetu wa kesho".
Kwa muda wa takribani masaa manne, watoto zaidi ya 150 walipata burudani mbalimbali ikiwa pamoja na michezo mbalimbali ya watoto kama “face painting”, mashindano ya kucheza muziki, na pia kupata nafasi ya kukutana na wafanyakazi wa Airtel, kumzungumza pamoja na kuwasisitiza watoto kuwa wasikivu shuleni ili kufanya vizuri kwenye masomo yao.
No comments:
Post a Comment