Wednesday, April 25, 2012



Mshauri wa Huduma Umoja wa Mataifa nchini Bw.George Otoo akifanya Presentantion juu ya ushiriki wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Mawasiliano kwa Maafisa Mawasiliano na Uhusiano waliohudhuria mafunzo hayo.


Na. Mwandishi wetu


Umoja wa Mataifa umesema Tanzania ni mshirika wake wa karibu katika jitihada za kukuza na kuendeleza sekta ya mawasiliano ambayo ndio kiungo muhimu katika kutimiza majukumu ya kila siku ya idara na taasisi mbali mbali za serikali na hata binafsi.


Akizungumza kwa niaba ya Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Bw. Alberic Kacou, wakati wa warsha ya siku moja ya mafunzo kwa maafisa uhusiano wa wizara na taasisi za kiserikali ilifanyika leo jijini Dar es Salaam, Kaimu wa Mwakilishi Mkazi Dkt. Julitta Onabanjo amesema UN inaitambua Tanzania kama nchi mfano wa kuigwa na itakayonufaika kwa kufuata mikakati ya kutimiza malengo.


Aidha amepongeza namna ushirikiano baina ya UN na Tanzania unavyokwenda haswa katika kutekeleza miradi mbalimbali ya mashirika tofauti ya Umoja huo na jinsi fedha za misaada zinavyotumika.


Naye Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu nchini Tanzania Bw. Salva Rweyemamu amesema mafunzo hayo yamefanyika wakati muafaka ambapo taifa linakabiliwa na changamoto mbali mbali katika sekta nyeti ya mawasiliano.


Amefafanua kuwa mawasiliano ni nyanja muhimu katika utawala na uongozi wa nchi na pia katika kuimarisha uhusiano wa kimatifa na nchi nyinginezo.


Mafunzo hayo ya siku moja yameandaliwa na United Nations communication Group kwa kupitia Ofisi ya Rais na kuwashirikisha maafisa uhusiano na maafisa mawasiliano kutoka Wizara, Idara na Taasisi kadhaa za serikali.


Bw. Owaiss Parray kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO) akifafanua Mipango ya kazi na njia za utekelezaji wake na jinsi zinavyohusiana na masuala ya mawasiliano.

Bw. Yusuph Al Amin kutoka Umoja wa Mataifa nchini akichambua vipengele vinavyohusiana na jinsi mawasiliano zinavyoweza kuchangia maendeleo.

Mtaalam wa masuala ya Teknolojia ya Habari Bw. Ayub Rioba akitoa somo kuhusiana na mipango na mikakati ya Serikali ya Mawasiliano ambapo pia alizungumzia juu ya umuhimu wa kufata maadili wakati wa kufanya mawasiliano katika semina ya mafunzo ya siku moja kwa Maafisa Mawasiliano wa Idara mbalimbali za Serikali.



Kaimu wa Mwakilishi Mkazi Dkt. Julitta Onabanjo akisoma hotuba wakati wa ufunguzi wa semina ya mafunzo kwa Maafisa Uhusiano wa Wizara mbalimbali nchini iliyoandaliwa na United Nations Communications Group kupitia Ofisi ya Rais iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.



Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu nchini Tanzania Bw. Salva Rweyemamu akitoa nasaha na shukrani kwa Umoja wa Mataifa kwa kuandaa mafunzo hayo ambayo amesema ni muhimu kwa ajili ya kuongeza ufahamu kwa maafisa mawasiliano na Uhusiano wa Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali.

Baadhi ya washiriki wa semina hiyo.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...