NYUMBA ZA SHIRIKA LA RELI, BANDARI MSIMBAZI DAR ZABOMOLEWA
Tingatinga likibomoa nyumba hizo.
Tingatinga likibomoa nyumba hizo.
MAMLAKA ya jiji la Dar es Salaam leo alfajiri ilianza kubomoa nyumba zilizokuwa za Shirika la Reli nchini na Bandari katika Mtaa wa Msimbazi, Kariakoo, karibu na Shule ya Msingi ya Uhuru, ili kupisha ujenzi wa kituo cha mabasi yaendayo kasi. Kazi hiyo iliyofanywa chini ya ulinzi mkali wa vyombo vya usalama, iliwaacha watu wengi waliokuwa wakiishi katika nyumba hizo kwa miaka mingi wakiwa katika majonzi makubwa ya kukosa mahali pa kukaa na kile walichosema ni kupoteza mali zao.
Hadi mtandao huu unakwenda mitamboni, kazi hiyo ilikuwa bado inaendelea, ikiwa imevuta watu wengi waliokuwa wakipita eneo hilo ambalo lina maduka na vituo vingi vya mabasi.
Tingatinga likibomoa nyumba hizo.
Vikosi vya zimamoto vikiwa tayari kutoa msaada wowote.
Mabaki ya nyumba iliyobomolewa.
Moja ya familia zilizoathirika na bomoabomoa hiyo.
Askari wakisimamia ubomoaji huo.
Eneo hilo lilikuwa limefungwa kwa wapita njia.
Moja ya nyumba ambazo zimebomolewa.

No comments:
Post a Comment