Sunday, March 25, 2012

IFA SOUND BAND:POPOTE UKUMBI KIKUBWA FEDHA IINGIE

VIJANA hawa wanaounda kundi la Ifa Sound Band, kutoka pande za Mbulahati jijini Dar es Salaam, juzikati walibahatika kukutana na Kamera ya Mateja20 maeneo ya Sinza Afrikasana Dar, na kuongea mawili matatu juu ya msimamo wa bendi hiyo, ambapo walisema kuwa wanamapungufu kibao yanayoikabiri bendi yao ikiwa pamoja na kupata mdhamini atakaye wanunulia vyombo na kuwatafutia Ukumbi maalum wa kufanyia sanaa yao kila siku.
Vijana hao waliendelea kusema kuwa tangu wameanzisha kundi hilo wamekuwa wakijipatia fedha kwa njia ya kuzunguka mitaani na kupiga muziki popote wapokuta mkusanyiko wa watu  na kujipatia  mapato kwa kutunzwa pale mtu anapofurahishwa na vionjo vyao.
Pamoja na hilo bado wanahitaji sapoti zaidi ili waweze kufikia malengo yao kwani vipaji wanavyo nakwamba  wana uhakika wakipata mtu wa kuwasaidia wanaweza kufanya vyema zaidi ya hivi sasa ambapo wanalazimika kupiga makopo na ngoma za kuunga unga ili wapate ridhi ya siku.
Kwa yoyote aliye tayari kuwasaidia anaweza kuwapigia kwa namba hii 0714576155.



Baadhi ya wapiga vyombo wa bendi hiyo wakichakalika kutoa burudani mbele ya Duka la Zizzou Fashion Sinza Afrikasana.



Vijana hao wakiimba na kucheza kwa pamoja.


Hii ndiyo set ya Drums yao wakichakalika kutafuta ridhiki.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...