Tuesday, March 27, 2012

HEBU TUJIKUBUSHE TENA KUHUSU SHOO YA JUMAPILI PALE DAR LIVE ILIVYOKUA

Kalala Junior (katikati) akiwa na wanenguaji wake wa Mapacha Watatu.

KITUO cha maraha cha Dar Live kilichoko Mbagala, Dar, kama kawaida, kilijaa kila aina ya chereko wakati wasanii wakongwe walipotoa shoo ya nguvu na kuwaacha wapenzi wa muziki wakiwa hawaamini usemi wa ‘Ya Kale Dhahabu’ au ‘Utu Uzima Dawa’. Burudani hiyo ilikwenda sambamba na muziki wa dansi kutoka bendi ya Mapacha Watatu.
Mnenguaji wa Mapacha Watatu akiwa kazini.

Mbunge wa Tabora Mjini, Aden Rage (kushoto), na Iddi Azzan wa Kinondoni, wote wa CCM walikuwa miongoni mwa umati uliofika Dar Live wikiendi.

Mwalimu wa ‘Kina Rihanna’, Dotto Villet ‘Spencer’ (mbele) akiwaongoza ‘wanafunzi’ wake waliotoa burudani katika kituo hicho cha maraha.

Wasanii Man Dojo (kushoto) na Domo Kaya wakiburudisha umati.

Umati uliofurika katika kituo hicho ukifurahia manjonjo ya mmoja wa Mabaga Fresh (kulia).

…Akiwapa ‘uchizi’ wa karibu na maikrofoni.

Kundi la Gangwe Mob likiongozwa na Inspeckta Haroun (katikati).

Wasanii Jay Moe (mbele) na Mansu Lee (kulia) wakipagawisha.

Msanii mkongwe, Dudu Baya (mbele) akiwa na msanii mwenzake.

….Akikongesha roho za mashabiki wake waliomfuata stejini.

Kalala Junior wa Mapacha Watatu akiwa juu kwa juu katika steji ya kisasa.


No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...