Wednesday, February 8, 2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

KILIMANJARO PREMIUM LAGER NA BASATA WATANGAZA WATEULE
WA VINYANG’ANYIRO VYA TUZO ZA MUZIKI TANZANIA (KILI TANZANIA
MUSIC AWARDS).
Dar es Salaam, Leo Jumatano 08 2012: Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia
yake ya Kilimanjaro Premium Lager kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa Tanzania
(BASATA) leo wametangaza rasmi wateule wa vinyang’anyiro 22 vya Tuzo za Muziki
Tanzania (Kilimanjaro Tanzania Music Awards).
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam leo, Meneja wa bia ya
Kilimanjaro Bwana George Kavishe alisema “Academy ilikaa mwisho wa wiki iliopita na
kufanya kazi ngumu na nzuri ya kuteua wasanii wa muziki waliofanya kazi nzuri na
zilizopendwa na kukubalika zaidi na wengi kwa mwaka 2011”.
Mchakato wa Academy ulisimamiwa na wasimamizi wa mahesabu na utawala INNOVEX
ili kuhakikisha zoezi linafanywa kwa uhuru na haki muda wote. George Kavishe aliongeza
“Kama tulivoahidi mwaka juzi na mwaka jana kwamba tuzo zitaendeshwa kisasa na
kitaalum ili kuzipatia haki na kutengeneza mazingira ya uwazi kwa wapenzi wa muziki
nchini. Tunaendeleza ahadi hii na ndio maana INNOVEX wameendelea kusimamia zoezi
hili la Academy pamoja na kura zote kwa mwaka huu tena.”
Kura za wana Academy ni siri na majibu ya wateule watano kwa kila kinyang’anyiro
hubaki siri ya INNOVEX hadi kutangazwa, halikadhalika na majibu ya kura za wananchi
za washindi.
Baraza la Sanaa Tanzania kupitia kwa mwakilishi wake Nd. Angelo Luhala ambaye ni
mratibu wa Tuzo za Muziki Tanzania, nalo limeipongeza Academy kwa kazi nzuri kwa
mara ingine na kuwasii wasanii kuyapokea matokeo na kushirikiana na waandaji katika
hatua zilizobakia ili kufanikisha tuzo hizi.
Hatua zifwatazo:
1. Semina ya Wasanii:
Wasanii wateule wa tuzo mbalimbali watapata semina elekezi kuhusu tuzo hizi na
kupata nafasi kuuliza maswali juu ya mchakato mzima wa kupata wateule na
taratibu zitakazofwata.
2. Kura.
Kura zitapigwa kwa muda wa wiki 7 kuanzia tarehe 13/ Feb - 06/ Apr Maelekezo
ya upigaji kura yatapatikana katika tovuti ya Kilimanjaro www.kilitimetz.com na
mitandao mingine pamoja na kwenye matangazo ya magazeti na vipindi mbali
mbali ya redio na TV.
3. Usiku wa utoaji Tuzo.
Kilimanjaro Tanzania Music Awards zatarajia kufanyika tarehe 14. Aprili. 2012
katika ukumbi wa Mlimani City. Taarifa zaidi zitafuata kupitia mitandao, redio na
TV mbali mbali.
-MWISHO



VIGEZO VINAVYOTUMIKA KUMPATA
MSHINDI WA TUZO ZA MUZIKI
(TANZANIA MUSIC AWARDS)
2
1. MTUMBUIZAJI BORA WA KIKE WA MUZIKI:
AWE HODARI WA KUIMBA NA KUCHEZA KWA
KIWANGO CHA JUU, HUKU AKISHIRIKISHA
WATAZAMAJI/WASIKILIZAJI WAKATI WOTE
AWEZE KUCHEZA NA KUVUTA PUMZI BILA
KUATHIRI UIMBAJI/UCHEZAJI
HODARI WA KULITAWALA JUKWAA
AWE NA NYIMBO ZILIZOREKODIWA NA KUSHIKA
CHATI ZA TV AU REDIO
ALIYEKUBALIKA ZAIDI MWAKA MZIMA/MAARUFU
2. MTUMBUIZAJI BORA WA KIUME WA MUZIKI:
§ AWE HODARI WA KUIMBA NA KUCHEZA KWA KIWANGO CHA
JUU, HUKU AKISHIRIKISHA WATAZAMAJI/WASIKILIZAJI
WAKATI WOTE
§ AWEZE KUCHEZA NA KUVUTA PUMZI BILA KUATHIRI
UIMBAJI/UCHEZAJI
§ HODARI WA KULITAWALA JUKWAA
§ AWE NA NYIMBO ZILIZOREKODIWA NA KUSHIKA CHATI ZA TV
AU REDIO
§ ALIYEKUBALIKA ZAIDI MWAKA MZIMA/MAARUFU
3. MWIMBAJI BORA WA KIUME:
§ UBORA NA UBUNIFU WA SAUTI/YENYE MVUTO
§ KIMO CHA SAUTI (RANGE) CHENYE UBORA
§ AWEZE KUTUMIA SAUTI YAKE (MINYUMBULIKO YA SAUTI JUU
NA CHINI)
§ AWEZE KUVUTA NA KUPUMUA PUMZI BILA KUATHIRI UIMBAJI
§ UNYOFU WA SAUTI ISIYO NA MIKWARUZO
§ LAZIMA AIMBE KWENYE FUNGUO
3
AWE NA NYIMBO ZILIZOREKODIWA NA KUSHIKA
CHATI ZA TV AU REDIO
ALIYEKUBALIKA ZAIDI KWA MWAKA
MZIMA/MAARUFU
4. MWIMBAJI BORA WA KIKE:
§ UBORA NA UBUNIFU WA SAUTI/YENYE MVUTO
§ KIMO CHA SAUTI (RANGE) CHENYE UBORA
§ AJUE KUTUMIA SAUTI YAKE (MINYUMBULIKO YA SAUTI JUU
NA CHINI)
§ AWEZE KUVUTA NA KUPUMUA PUMZI BILA KUATHIRI UIMBAJI
§ UNYOFU WA SAUTI ISIYO NA MIKWARUZO
§ LAZIMA AIMBE KWENYE FUNGUO
§ AWE NA NYIMBO ZILIZOREKODIWA NA KUSHIKA CHATI ZA TV
AU REDIO
§ ALIYEKUBALIKA ZAIDI KWA MWAKA MZIMA/MAARUFU
5. WIMBO BORA WA TAARAB:
§ UWE UMETUNGWA NA KUIMBWA KWA UFUNDI
§ UWE NA UJUMBE MZURI WA KUASA, KUONYA, KUFUNDISHA
(FURAHA AU HUZUNI) NA KUBURUDISHA
§ USIWE NA LUGHA ISIYOFAA (MATUSI).
§ UWE UMEIMBWA KWENYE FUNGUO
§ UWE UMESHIKA CHATI KATIKA TV AU REDIO KWA MUDA
MREFU
§ UWE UMEIMBWA KWA HISIA KULINGANA NA MANENO
YALIYOMO KATIKA WIMBO
§ UWE UMEKUBALIKA NA MAKUNDI YOTE YA JAMII
4
6. WIMBO BORA WA MWAKA:
UWE UMETUNGWA NA KUIMBWA KWA UFUNDI
UWE NA UJUMBE MZURI WA KUASA, KUONYA,
KUFUNDISHA (HUZUNI AU FURAHA) NA
KUBURUDISHA
UWE UMEIMBWA KWA HISIA KULINGANA NA
MANENO YALIYOMO KATIKA WIMBO
USIWE NA LUGHA ISIYOFAA (MATUSI)
UWE UMEIMBWA KWENYE FUNGUO
UWE UMESHIKA CHATI KATIKA TV AU REDIO
KWA MUDA MREFU
UWE UMEKUBALIKA NA WENGI/MAARUFU
7. WIMBO BORA WA KISWAHILI (BENDI):
§ UWE UMETUNGWA NA KUIMBWA KWA KISWAHILI NA KWA
UFUNDI
§ UWE UMEIMBWA KWENYE FUNGUO
§ UWE UMEIMBWA KWA HISIA KULINGANA NA MANENO
YALIYOMO KATIKA WIMBO
§ UWE NA UJUMBE MZURI WA KUASA, KUONYA, KUFUNDISHA
(FURAHA AU HUZUNI) NA KUBURUDISHA
§ USIWE NA LUGHA ISIYOFAA (MATUSI)
§ UWE UMESHIKA CHATI KATIKA TV AU REDIO
§ UWE UMEKUBALIKA NA WENGI/MAARUFU
5
8. WIMBO BORA WA R&B:
UWE UMEPIGWA KATIKA MIONDOKO YA R&B
UWE UMETUNGWA NA KUIMBWA KWA UFUNDI
KWENYE FUNGUO
UWE UMEIMBWA KWA HISIA KULINGANA NA
MANENO
UWE NA UJUMBE MZURI WA KUASA, KUONYA,
KUFUNDISHA (FURAHA AU HUZUNI) NA
KUBURUDISHA
UWE UMESHIKA NAFASI ZA JUU KWENYE CHATI
ZA MUZIKI ZA VITUO MBALIMBALI VYA TV AU
REDIO
USIWE NA LUGHA ISIYOFAA (MATUSI)
UWE UMEKUBALIKA NA WENGI/MAARUFU
9. WIMBO BORA WA HIP HOP:
§ UWE UMEPIGWA KATIKA MIONDOKO HALISI YA HIP HOP
§ MWIMBAJI AWE AMEGHANI KWA HISIA KULINGANA NA
MANENO YENYE VINA NA MIZANI
§ UWE UMETUNGWA KWA GHANI YENYE UFUNDI KWENYE
FUNGUO
§ UWE UMESHIKA NAFASI ZA JUU KWENYE CHATI ZA MUZIKI
ZA VITUO MBALIMBALI VYA TV AU REDIO
§ UWE NA UJUMBE MZURI WA KUONYA, KUASA, KUFUNDISHA
(HUZUNI AU FURAHA) NA KUBURUDISHA
§ USIWE NA LUGHA ISIYOFAA (MATUSI)
§ UWE UMEKUBALIKA NA WENGI/MAARUFU
6
10. WIMBO BORA WA REGGAE:
UWE NA UJUMBE MZURI WA KUONYA, KUASA,
KUFUNDISHA (FURAHA AU HUZUNI) NA
KUBURUDISHA
UWE KATIKA MIONDOKO HALISI YA MUZIKI WA
REGGAE
UWE UMEKUBALIKA NA WENGI
USIWE NA LUGHA ISIYOFAA (MATUSI)
UWE UMETUNGWA NA KUIMBWA KWA UFUNDI
UWE UMEIMBWA KWENYE FUNGUO
11. WIMBO BORA WA RAGGA/DANCEHALL:
§ UWE UMEKUBALIKA NA WENGI
§ UWE KATIKA MIONDOKO HALISI YA MUZIKI WA
RAGGA/DANCEHALL
§ UWE NA UJUMBE MZURI WA KUASA, KUONYA, KUFUNDISHA
(FURAHA AU HUZUNI) NA KUBURUDISHA
§ USIWE NA LUGHA ISIYOFAA (MATUSI)
§ UWE UMETUNGWA NA KUIMBWA KWA UFUNDI
§ UWE UMEIMBWA KWENYE UFUNGUO
12. RAPA BORA WA MWAKA (BENDI):
§ AWE MWENYE UBUNIFU WA MANJONJO KATIKA MTIRIRIKO
WA KUIMBA KULINGANA NA MDUNDO
§ AWE MWENYE MVUTO KATIKA KUFOKA NA ANAYEKUBALIKA
NA WENGI
§ AWE NA UWEZO WA KUTAWALA JUKWAA NA
KUWASHIRIKISHA WATAZAMAJI
7
13. MSANII BORA WA HIP HOP:
AWE MAHIRI WA KUFOKA KWENYE VINA NA
MIZANI
AWEZE KUTUMIA SAUTI YAKE (MINYUMBULIKO
YA SAUTI JUU AU CHINI)
AWEZE KUVUTA NA KUPUMUA PUMZI BILA
KUATHIRI GHANI ZAKE.
LAZIMA AWE MCHAGUZI MZURI WA TUNI
(MELODY)
LAZIMA AGHANI KWENYE FUNGUO
UWE NA UJUMBE MZURI WA KUASA, KUONYA,
KUFUNDISHA (FURAHA AU HUZUNI) NA
KUBURUDISHA
ASITUMIE LUGHA ISIYOFAA (MATUSI)
14. WIMBO BORA WA AFRIKA MASHARIKI:
§ UWE UMETUNGWA NA KUIMBWA KWA UFUNDI NA KWENYE
FUNGUO
§ UWE UMESHIKA NAFASI ZA JUU ZA CHATI MBALIMBALI ZA
VITUO VYA REDIO AU TV HAPA NCHINI
§ UWE NA UJUMBE MZURI WA KUASA, KUONYA, KUFUNDISHA
(FURAHA AU HUZUNI) NA KUBURUDISHA
§ USIWE NA LUGHA ISIYOFAA (MATUSI)
§ UWE UMEIMBWA KWA HISIA KULINGANA NA MANENO
§ UWE UMEKUBALIKA NA WENGI/MAARUFU
§ USIMILIKIWE NA MSANII WA TANZANIA.
8
15. MTUNZI BORA WA MWAKA
AWE MBUNIFU NA MWENYE KUTUNGA MELODI
NZURI
AWE ANAJUA KUPANGA IPASAVYO MELODI
ZAKE KWA MTIRIRIKO MWANANA
AWE ANAJUA KUPANGA MASHAIRI YENYE VINA
MUAFAKA
MAUDHUI AU UJUMBE UNA MAANA GANI/UZITO
UPI KUELIMISHA, KUKOSOA, KUELEKEZA JAMII
KATIKA MAISHA YAO YA KILA SIKU
AWE NI MTUNZI HALISI WA WIMBO
16. MTAYARISHAJI (PRODUCER) BORA WA NYIMBO WA MWAKA:
§ AJUE KUPANGA MUZIKI KWA KUFANYA ULINGANIFU WA ALA
NA SAUTI MBALIMBALI
§ AJUE JINSI YA KUTAYARISHA/KUPANGA ALA, UIMBAJI NA
KUTOA KWENYE VIBEBEA SAUTI.
§ AWE AMETOA NYIMBO NYINGI ZILIZOPATA UMAARUFU NA
KUKUBALIKA NA WENGI/MAARUFU.
17. VIDEO BORA YA MUZIKI YA MWAKA (MOST POPULAR MUSIC
VIDEO OF THE YEAR)
§ IWE NA MVUTO NA IKUBALIKE NA WATU WENGI/MAARUFU
§ IWE IMEOMBWA NA WATAZAMAJI NA KUSHIKA NAFASI ZA
JUU KWENYE CHATI ZA JUU ZA TELEVISHENI MBALIMBALI NA
VYANZO VINGINE KAMA U-TUBE, BLOGS NK.
§ IWE NA MTIRIRIKO WA MATUKIO YANAYOENDANA/RANDANA
NA UJUMBE WA KWENYE NYIMBO
§ IWE NA MVUTO NA UBORA WA PICHA NA IKUBALIKE NA
WATU WENGI/MAARUFU.
§ MSANII/WASANII WAWE NA MVUTO NA STADI YA MUZIKI
WENYE KUKUBALIKA NA JAMII KATIKA VIDEO HIYO.
9
MSANII/WASANII WAWE NA MAVAZI YA HESHIMA
NA UCHEZAJI USIOWADHALILISHA WAO NA
WATAZAMAJI.
18. WIMBO BORA WA AFRO POP:
UWE UMEPIGWA KATIKA MIONDOKO HALISI YA
KIAFRO POP.
UWE UMETUNGWA NA KUIMBWA KWA UFUNDI
NA KWENYE UFUNGUO
UWE UMESHIKA NAFASI ZA JUU KATIKA CHATI
MBALIMBALI ZA VITUO VYA REDIO AU TV
UWE NA UJUMBE MFUPI WA KUASA, KUONYA,
KUELIMISHA (FURAHA AU HUZUNI) NA
KUBURUDISHA.
USIWE NA LUGHA ISIYOFAA (MATUSI)
UWE UMEKUBALIKA NA WENGI MAARUFU
19. WIMBO BORA WA ZOUK/RHUMBA
§ UWE UMEKUBALIKA NA WENGI
§ UWE UMESHIKA NAFASI ZA JUU KATIKA CHATI MBALIMBALI
ZA TV AU REDIO
§ UWE UMEPIGWA KATIKA MIONDOKO HALISI YA
KIZOUK/RHUMBA.
§ UWE NA UJUMBE MZURI WA KUASA, KUONYA, KUELIMISHA
(FURAHA AU HUZUNI) NA KUBURUDISHA.
§ USIWE NA LUGHA ISIYOFAA (MATUSI).
§ UWE UMETUNGWA NA KUIMBWA KWA UFUNDI.
§ UWE UMEIMBWA KWA HISIA KULINGANA NA MANENO
YALIYOMO KATIKA WIMBO.
10
20. WIMBO BORA WENYE VIONJO VYA ASILI YA
KITANZANIA
UWE NA UJUMBE MZURI WA KUASA, KUONYA,
KUELIMISHA (FURAHA AU HUZUNI) NA
KUBURUDISHA
USIWE NA LUGHA ISIYOFAA (MATUSI)
UWE NA MAADILI YA ASILI YA KITANZANIA
UWE UMEIMBWA KWA MAHADHI NA MIRINDIMO
YENYE VIONJO VYA ASILI.
UWE UMETUNGWA NA KUIMBWA KWA UFUNDI
UWE UMEIMBWA KWENYE FUNGUO
21. MSANII BORA CHIPUKIZI ANAYEIBUKIA
§ AWE NA UBUNIFU BORA WA SAUTI.
§ AWE AMETOA WIMBO AU NYIMBO ZILIZOKUBALIKA NA
WENGI
§ WIMBO AU NYIMBO ZAKE ZIWE ZIMEPIGWA KATIKA VYOMBO
VINGI VYA REDIO AU TV.
§ AWE NA WIMBO ULIOSHIKA NAFASI ZA JUU KWENYE CHATI
ZA MUZIKI KATIKA VITUO VYA TELEVISHENI NA REDIO.
§ AWE AMEKUBALIKA NA WADAU WA MUZIKI.
§ AJUE KUTUMIA SAUTI YAKE (MNYUMBULIKO WA SAUTI JUU
NA CHINI).
§ AWE MCHAGUZI MZURI WA TUNI (MELODY)
§ AIMBE KWENYE FUNGUO
§ AWE AMEIMBA KWA HISIA KULINGANA NA MANENO KWENYE
WIMBO.
11
22. WIMBO BORA WA KUSHIRIKIANA/KUSHIRIKISHA
UWE WIMBO WA MSANII AU KIKUNDI NA
KUSHIRIKISHA MSANII AU KIKUNDI
UWE NI WIMBO ULIOTUNGWA NA KUIMBWA KWA
USHIRIKIANO WA MSANII NA MSANII, KUNDI NA
KUNDI AU KUNDI NA MSANII.
UWE NA UBUNIFU BORA WA MPANGILIO WA
SAUTI
UWE WIMBO ULIOSHIKA CHATI ZA JUU KATIKA
VITUO VYA REDIO AU TV
UWE UMEKUBALIKA NA WENGI/MAARUFU.
23. MDAU WA MUZIKI ALIYEFANIKISHA MAENDELEO YA MUZIKI (HALL
OF FAME):
§ MSANII/MTU BINAFSI/KAMPUNI YENYE MCHANGO MKUBWA
KWENYE TASNIA YA MUZIKI NA UNAOTAMBULIWA NA JAMII
NA WADAU WA MUZIKI KWA KIPINDI KIREFU.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...