Wednesday, January 25, 2012


RAY THE GREATEST NDANI YA CHINA
Kama kawaida wadau wangu nilivyowahidi kuwa nitawaletea matukio ya uku niliko, Cha kwanza kabisa nimekuja uku kwa ajili ya kuongeza vifaa vya kampuni ili mwaka huu tufanye mapinduzi makubwa katika tasnia yetu. Mimi sisemi sana wewe mwenyewe utajionea mambo yatakavyobadilika mwaka huu,pili kuna sinema nayotegemea kupiga katika nchi hizi tatu nilizowatajia China,Hong kok pamoja na Thailand katikati ya mwaka huu twende pamoja.


Hapa nikiwa na mshikaji wangu Choba katika maswala mazima ya kununua camera za still picture


Hapa pia nikiwa na kijana wangu Kounja, huyu kijana jamani hachagui chakula chochote yeye poa tu mpaka supu ya nyoka kijana twende ni hatari sana huyu kijana cheki anvyonikata jicho


Ili ni soko kubwa la simu ni original tu hakuna feki lakini ukitaka soko la feki nalo lipo pia


Baadhi ya mizigo yangu ikiwa ipo katika chumba nilichofikia


Kama kawaida mambo yakipamba moto
Wadau chumba changu kilikuwa kiko lafu sana kwa ajili mizigo ilikuwa ni mingi sana
Hapa nikiangalia camera ya still picture nikipata maelekezo kutoka kwa mtaalam toka Congo niliyekutananae uko uko wa katikati ,kwa kweli akinisaidia sana...
Mizigo yangu ikiwekwa sawa na wachina wenye duka hapo hakuna boss wao ndio wauzaji na wao ndio wafunga mizigo,Hawa jamaa wapo makini sana na kazi na ndio maana sikuku yao ya mwaka mpya wanakaa mwezi mzima bila kufanya kazi yoyote kama muda huu ukienda China utakuwa umepata hasara hakuna duka la shughuli yoyote inayoendelea kwa sasa..
Picha ya pamoja rafiki yangu Choba na wachina wenye duka
The greatest naye akipata picha ya kumbukumbu
Nikikagua vifaa ukiingia kwenye duka ili ukosi kitu cha video production
Hapa ni hatari wewe angalia mwenyewe .
Dolly nimenunua hela nyingi kidogo ni special kwa ajili ya shorts flani hivi ambazo mtaziona kwenye movie mpya ambazo nitawatajia
Taa mpya pia nimenunua kwa ajili ya kuongeza ubora hizi ni taa bora sana kwa matumizi yetu


Upande wa camera
Duka zima linavyoonekana sijui hata haya maandishi yana maana gani?kwa ndugu zangu wachina watakuwa wanajua maana yake. Haya ni baadhi tu ya matukio bado mengi nitawaletea na usiku huu nategemea kuondoka kurudi bongo hapa napowablogisha nipo uwanja wa ndege

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...