Friday, January 27, 2012




MWIMBAJI WA NYIMBO ZA INJILI LILIAN AELEZA MATATIZO ANAYOYAPATA KATIKA MAISHA YAKE, ASEMA, "USIONE MTU AMEPENDEZA, HUJUI KINACHOMSUMBUA MOYONI MWAKE"

Lilian ni dada aliyemaliza kidato cha sita katika shule ya Baobab,Bagamoyo mwaka 2011 na kutofanya vizuri katika mtiahani wa mwisho wa kuhitimu kidato cha sita kutokana ukatili wa baba yake kwa watoto wa kike, na alipokuwa kidato cha nne alipata daraja la pili...Pia aeleza hasara za kuwa na mahusiano ya kimapenzi mashule..na yeye alipitia hayo akapatwa pigo ambalo hatalisahau maishani mwake. Lilian alikumbwa na mengi na baya zaidi ni kushauriwa na rafiki yake aliyekutana naye katika facebook na kumshauri awe msagaji Mbali na hapo Lilian anaelezea kipaji chake alichonacho.

Na haya yalikuwa mahojiano

Ni vizuri kuishi na wanyama wanaonifanya niwe raha kuliko wandamu.
RUMA: Hello Lilian, Shalom
LILIAN: Shalom

RUMA: Tungependa kujua majina yako ambayo yako katika passport yako?
LILIAN: Ok, Lilian Elidadi Flikley

RUMA: Jina lako zuri sana..swali la uzushi kwanini Flikley..mbona limekaa kizungu zaidi?
LILIAN: Hahahaha asante
               Yeah it's ma grand paz name
               He is just a black
               But long time the Germans used to be there

RUMA:  Mhhh...lazima kuna sababu..ok tuache hilo..Mko wangapi katika familia yenu?
LILIAN:  5 to  mum..10 to dad, Lol many
           
RUMA: Waoh..kweli your dady alikuja kuijaza dunia..wonderful...nipe mchakato wa gender
                  nikimaanisha wangapi wanaume na wangapi wa kike?
LILIAN: 4 galz 6 boys

RUMA: Wewe ni wangapi katika familia hiyo kubwa?
               Faida ni kwamba mzaliwa wa kwanza hudhaminiwa sana na kwamba mimi ni 
               kiongozi katika familia na mimi ni kioo chao.

RUMA: Mhhh..kweli Lilian unajua mambo..kwahiyo wewe unataka uwe katika pande ipi kati
               ya hizo point mbili umetoa?
LILIAN: On the positive side 4sure

RUMA: Ok vizuri sana dada yangu..unafikiri ni mambo gani umefanya mpaka sasa kwa
               wdogo zako ambayo ni positive na wataweza kukuiga?

LILIAN: Nimekua mwimbaji nikawa mtunzi nao wakanifuata, Nimekua msafi sana i mean
                hygienically nao wakanifwata...

RUMA: Oooh wonderful..kwahiyo wewe ni mwimbaji..unaimba nyimbo za upande
               upi..nikimaanisha kijamii au kikristo?
LILIAN: Kikristo zaidi. Za kijamii zipo ila na ukristo ndani yake

RUMA: Hongera sana na hao waliokufuata katika uimbaji wanaimba muziki wa aina gani?
LILIAN: Kikristo zaid


RUMA: Turudi kwako..katika nyimbo za kijamii unalenga katika kuelimisha jamii kwa kutoa
               ujumbe wa aina gani hasa?
LILIAN: Urafiki wa uongo, na ndoa,
               Katika mafanikio ni Mungu 2 amewawezesha sio kwa nguvu zao tu

RUMA: Mh dada uko juu..wewe ni wakipekee...swali la uzushi..umeolewa au unamchumba
               mpaka umefikia kutoa ujumbe wa aina hiyo?
LILIAN: Sijaolewa,na sinamchumba ila nilikuwa nae.

RUMA: Tuelezee kwanini umeimba kuhusu mapenzi na ndoaLILIAN: Kuhusu ndoa
                Ninaishi na wazazi wangu ambapo kuna matatizo mengi ya ndoa ninayaona ndo 
               mana nimetunga wimbo wa ndoa.
                Kuhusu urafiki wa uongo,nilikuwa na rafiki aliyemjua mpenzi wangu huyo rafiki
                alimwunganisha msichana mwingine kwa mchumba wangu.
RUMA: Pole sana hilo swala la rafiki yako kuharibu uchumba wenu limenigusa na kuniumiza
                sana..natumaini uliumia sana..kwahiyo hii imekufanya ukaanza kutunga nyimbo za
                aina hiyo? Ulifanyeje baada ya uchumba wenu kuvunjika?
LILIAN: Nikaachana nae coz kama kweli alikuwa ananipenda asingekubali kuunganishwa na
                msichana huyo.
                Yule msichana bahati nzuri alikuwa hajui kuwa dat boy ni mchumba wangu.
                Nilisoma loyola na huyo mpenzi wangu so yule msichana was a friend of mine nat
                that close. So akaja kuniuliza unamfahamu huyu kaka anaitwa..alisoma loyola?
                nikamjibu yes ndo akaniambia anamtaka na rafiki yangu ndo anawaconect
                Me nikamwambia mbona ni bf wangu? Akashtuka akashangaa na yeye akamwacha
                akaluz kote.

RUMA: Inaumiza na inafurahisha..rafiki yako aweza kuwa adui yako..wewe ulimchuliaje
                huyo rafiki yako na vipi mahusiano yenu mpaka sasa?
LILIAN: Nilimchukulia vibaya ila alikana but nimemsamehe We are nat that close again ni
                rafiki wa kawaida tu.

RUMA: Pole sana..ni kipindi gani ulianza mahusiano na huyo mkaka asiye na msimamo
                na nanitwa nani?
LILIAN: Nilikuwa f6 (form six), Ilichukua kama miezi mingi2

RUMA: Ni mwaka gani umemaliza kidato cha sita?
LILIAN: Mwaka Jana 2011, Feb

RUMA: Inasemekana kisheria mwanafunzi haruhusiwi kuwa na mchumba wakati bado
                ni mwanafunzi..wewe ilikuwaje?

LILIAN: Hahaa
                I dnt know but niliweza kujicontrol those are natural things sometimez u fil like
                having one.

RUMA: Waoh..let us go back...Swala la kuwa na mchumba wakati unasoma bado
                halikukuathiri katika masomo yako? Naomba utoe ukweli kuwafundisha na wengine
                wanakuwa na wachumba mashuleni.
LILIAN: Yeah kuathiri kupo.
                Kupoteza muda mwingi kumwaza umpendae nakushindwa kusoma kumbe mwanaume
                mwenyewe hana habari na mimi.
                Lol

RUMA:Nini unaweza kuwashauri wadada kama wewe waliopitia haya uliyopitia...?
LILIAN: Kuachana na uhusiano wa kimapenzi wakiwa shuleni.

RUMA: Turudi katika uimbaji wako..Nini kimekusukuma kuimba nyimbo zinazohusu ndoa
                dada wa Yesu?
LILIAN: Naona kwa wazazi wangu. na familia yetu

RUMA: Imekuaje tena huko dada yangu..inaonekana unapitia katika mapito fulani?
LILIAN: Yeah yaani naona live Mungu anamakusudi yake kwanini napitia yote hayo
                Ni mambo ya kawaida lakini.

RUMA: Ningeomba kujua hayo unayopitia dada yangu ili jamii ijue na inaweza kuguswa
                na kutafuta njia za kukutoa dada yangu
LILIAN: Ok kivipi?

RUMA: Tunataka kujua ni kwanini unaimba nyimbo za ndoa..vitu gani vilikugusa mpaka
                ukafikia kuimba nyimbo hizo...umetueleza kuwa ni kutokana na familia yako...lakini
                kivipi?
LILIAN: Ok
Wanagombana kila siku

RUMA: Tunataka kujua ni kwanini unaimba nyimbo za ndoa..vitu gani vilikugusa mpaka
                ukafikia kuimba nyimbo hizo...umetueleza kuwa ni kutokana na familia yako...lakini
                kivipi?
LILIAN: Ok, Wanagombana kila siku
                Ubaguzi wa watoto i mean kijinsia kusema watoto wakike sio ki2
                Kumpiga mama akiwa mjamzito na miezi tisa mimi na mama tukajificha chini
                ya kitanda
                Kuzuia ndugu wa mama kuja nyumbani
                Kutufukuza nyumbani..sisi wakike
                Pamoja na mama
                Baba Kumwacha mama hospital baada ya kusikia kazaa wa kike
                Yapo mengi sana
                Baba hapendi niimbe gospel
                Anasema sikufanya vizuri 6 coz ya kuimba gospel
                Kumdhalisha mke wake kwa watu.
                Cnt say ol ni mapito rulea

RUMA: (Nikanyanyua simu yangu na kumpigia kuhakikisha kuwa huyu mtu ninaye-chart ni kweli.
Baada hapo niliamua kumuomba twendelee na mahojiano kipindi kijacho. Nilishindwa kuendelea kutokana na uchungu nilioupata. Nikampigia mtangazaji wa Praise Power, Jimmy ili afanye naye Interview katika kipindi cha Booster cha usiku)

TUTAENDELEA NA MAHOJIANO HAYO KIPINDI KIJACHO..ENDELEA KUTEMBELEA BLOG HII....

WASILIANA NA LILIAN KWA SIMU: 0653 005202













No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...