Friday, January 20, 2012

FM ACADEMIA WAWASHA MOTO  DAR LIVE MBAGALA

a
BENDI ya muziki wa dansi nchini ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’, usiku wa kuamkia leo walifanya makamuzi ya kufa mtu ndani ya ukumbi wa kisasa wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar es Salaam. 

Wanamuziki hao pia walisifia mandhari ya ukumbi na jukwaa la muziki na kuahidi watahakikisha wanafanya shoo katika ukumbi huo kila siku ya Alhamisi kutokana na wingi wa mashabiki waliohudhuria. 

Nyoshi El-Saadat (kushoto), akibadilishana mawazo na baadhi ya wanenguaji wake.

Baadhi ya mashabiki waliohudhuria ukumbini hapo wakiserebuka.

Mmoja wa waimbaji wa bendi hiyo ‘akigonga’ kongoro ukumbini hapo.


Mwanamuziki wa Bendi ya Msondo Ngoma, Hassani Moshi ‘TX Junior’ (katikati), akishuhudia shoo hiyo na rapa wa bendi hiyo,  Toto Kalala (kushoto), na mratibu wa shoo hiyo Juma Mbizo


Wanenguaji wote wa bendi hiyo wakiwa kwenye pozi la pamoja

Rais wa bendi hiyo, Nyoshi El- Saadat (wa pili kushoto), akiongoza safu ya waimbaji na mnenguaji machachari, Suzan Chubwa (Queen Suzi, katikati).

Warembo wakifuatilia shoo hiyo.


Baadhi ya wanenguaji wa kike wa bendi hiyo wakiwa katika pozi.

Rapa Toto Kalala akiwa majukumu yake.

Rapa Toto Kalala akiwa majukumu yake.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...