Thursday, January 26, 2012


DKT BILAL ZIARANI WILAYA YA MUHEZA – TANGA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwasili eneo la CCM Wilayani Muheza na kupokelewa na Vijana shupavu wa CCM.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Ghari Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wa CCM Wilaya ya Muheza, alipowasili eneo hilo kwa ajili ya kupokea taarifa ya utendaji kabla ya kuanza kukagua baadhi ya miradi ya maendeleo akiwa katika ziara yake Wilayani Muheza Mkoa wa Tanga jana Januari 25, 2012.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka Jiwe la Msingi katika Soko jipya la Michungwani, wakati akiwa katika ziara yake ya Wilaya ya Muheza, jana Januari 25, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Muheza waliokuwa wamekusanyika nje ya ofisi ya CCM wakimtaka kuzungumza nao baada ya kupokea taarifa ya utendaji kutoka kwa viongozi wa CCM wa Wilaya hiyo, wakati akiwa katika ziara yake ya Wilaya ya Muheza Mkoa wa Tanga jana Januari 25, 2012.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka jiwe la Msingi katika Shule ya Sekondari ya Seminari ya Living Stone, jana Januari 25, 2012, wakati akiwa katika ziara yake ya Wilaya ya Muheza Mkoa wa Tanga.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wananfunzi wa Kidato cha kwanza wa shule ya Sekondari Seminari Living Stone, baada ya kuweka Jiwe la Msingi katika shule hiyo akiwa katika ziara yake ya Wilaya ya Muheza mkoa wa Tanga jana, Januari 25, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipanda mti wakati alipotembelea Msitu wa asili wa Hifadhi wa Amani, akiwa katika ziara yake ya Wilaya ya Muheza Mkoa wa Tanga, jana Januari 25, 2012.


No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...