Wednesday, January 11, 2012

DIDA KUDONDOKA BONGO IJUMAA HII
Mtangazaji mahiri wa kituo cha Times FM, kupitia kipindi cha Mitikisiko ya Pwani, Khadija Shaib 'Dida wa G' anatarajiwa kudondoka Bongo Ijumaa hii akitokea Hong Kom China, alikoenda kwaajili ya mambo yake ya kibiashara  ikiwa ni pamoja na kwenda kutafuna bata za kutosha nchini Afrika Kusini ambako alipitia kabla ya kwenda Hong Kom.
Akizungumza kwa njia ya simu nchini humo na Mateja20, alisema kuwa anatarajia kudondoka Bongo siku hiyo tayari kwa kukabiliana na majukumu yake ya kila siku.
"Nitaingia Ijumaa maana nimewamisi ile mbaya mashabiki wa kipindi changu, hivyo nitakapofika tu j3 nitafanya suprise ya aina yake na kila mmoja atakubaliana na mapumziko yangu, kwani kuna vitu kibao vipya nimewaandalia," alisema Dida.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...