Na Fredy Mgunda, Iringa
Mbunge wa Mufindi Kusini Mahamood
Mgimwa ameweza kugawa vifaa mbalimbali vya michezo kama alivyowahidi kwa Vijana
na timu za Jimbo hilo huku akitaka
michezo yote kuendelezwa.
Mgimwa ametekeleza ahadi hiyo katika
Vijiji mbalimbali vinanvyounganisha Jimbo hilo la Mufindi Kusini katika ziara
yake inayoendelea ya kuwashukuru wananchi wake kwa kuweza kumchagua kwa kura
nyingi na kwenda kuwaakilisha Bungeni.
Akielezea wakati wa kutoa vifaa hivyo
vya Michezo, Mgimwa amebainisha kuwa, vifaa hivyo anavitoa ni kutokana na ahadi yake yeye ka,a Mbunge aliiahidi kwa Vijana hao
kuwapatia vifaa hivyo huku baadhi yao
pamoja na timu zilimuomba vifaa hivyo ambapo sasa anafanya kutekeleza.
“Niliahidi kuleta vifaa vya Michezo
kwa kila Kata. Lakini pia mimi mwenyewe niliwaahdi kuwaletea vifaa nan leo hii
natimiza ahadi yangu kwenu.” Alieleza Mgimwa.
Mgimwa ameongeza kwa kusema ameamua
kutoa vifaa hivyo Kwa lengo la kusaidia Serikali katika juhudi za kuinua
michezo lakini pia nisehemu ya Kazi zake kama Mbunge.
![]() |
Mbunge wa Mufindi Kusini Mahamood
Mgimwa akikabidhi vifaa vya mchezo wa mpira wa miguu akiwa sambamba na
mwenyekiti wa ccm wilaya ya mufindi Yohanes Kaguo.
|
Amesema kuwa michezo licha ya kujenga
utimamu wa mwili lakini pia ni ajira huku akitoa mfano Kwa Mbwana Samatta
anavyofanikiwa na leo anakipiga Ulaya.
Vifaa hivyo vya michezo ikiwemo seti
nzima za Jezi na mipira ya kuchezea ni
hatua ya kuinua na kuendeleza vipaji kwa Vijana wa Jimbo hilo ambao wamekuwa na
shahuku kubwa ya kuibua vipaji vyao vya mpira wa miguu.
Aidha, amewataka Vijana hao kuwa na
tabia ya kufanya mazoezi ya mara kwa mara kwani yatawasaidia kufanya vizuri
katika mpira wa miguu na pia mazoezi ni afya huku kipaji cha mpira wa miguu
kikiwa ni ajira kwao pia endapo michezo itaendelezwa zaidi hasa kwa vijana
walio pembezoni.
No comments:
Post a Comment