Tuesday, April 19, 2016

AZAM TV YAZINDUA KIWANDA CHA FILAMU NA TAMTHILIA YA TAXI


Kutoka kushoto ni muigizaji mahiri wa filamu Bongo, Suzan Lewis ‘Natasha’, Mkuu wa Masoko na mauzo wa Azam, Mrope Kiwanga, Msimamizi Uzalishaji wa kipindi cha Sinema Zetu, Zamaradi Nzowa,  Mhadhiri Msaidizi wa UDSM, Issa Mbura na Meneja Mipango, Fatma Mohamed, wakikata keki ya uzinduzi wa projekti ya Kiwanda cha Filamu na kipindi kipya cha Taxi kitakachokuwa kikirushwa hewani kupitia Channel 103 ya Sinema Zetu ya Azam TV ikiwa ni moja ya projekti mpya.


AZAM TV kupitia chaneli yake ya Sinema Zetu, mapema leo imezindua rasmi ‘projekti’ iliyopewa jina la Kiwanda cha Filamu, na kipindi kipya kiitwacho Taxi,  vyenye lengo la kuibua vipaji vya wasanii wa maigizo  na wapiga picha za video chipukizi.
Projekti hiyo ambayo ilianzishwa mwanzoni mwa Machi mwaka huu ilitoa furasa kwa watu mbalimbali ambao wangependa kushiriki kutuma kazi zao na wamepatikana zaidi ya washiriki 200.
Akizungumza na wanahabari katika uzinduzi huo kwenye ofisi za Azam zilizoko eneo la Tazara jijini Dar, Msimamizi wa Uzalishaji wa Sinema Zetu, Zamaradi Nzowa, alisema washiriki hao watawachuja chini ya majaji akiwemo muigizaji wa siku nyingi hapa nchini, Suzan Lewis ‘Natasha’, ili kuwapata  washiriki 22.
Baada ya kupatikana, watapatiwa mafunzo mafupi kisha wao pamoja na mastaa wa filamu hapa nchini watashiriki kwenye tamthilia itakayojulikana kwa jina la Taxi.
Nzowa alisema: “Washiriki ni kuanzia umri wa miaka 18 na kesho Jumatano pale Coco Beach ndipo tutaanza kufanya mchujo wa awali ambapo mpaka mwisho tunatarajia kupata waigizaji 20 na wapiga picha wawili ambao watashiriki kwenye tamthilia ya Taxi ambayo itazinduliwa Julai mwaka huu na itakuwa ikionyeshwa katika chaneli yetu ya Sinema Zetu.”

Mrope Kiwanga, akifafanua zaidi namna projekti hiyo itakavyonufaisha watu wengi.

Zamaradi Nzowa akikata keki kuashiria uzinduzi rasmi wa projekti hiyo.

Muigizaji Suzan Lewis ‘Natasha’, (kushoto) akimlisha keki msanii na mtangazaji mahari Bongo, Daniel Kijo.

Baadhi ya waandishi wa habari na wahusika wa tukio hilo wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa uzinduzi huo.

Muigizaji Issa Mbura (kushoto) akimlisha keki Natasha.

Mwandishi wa gazeti la Championi, Mohamed Mdose (kushoto) akilishwa keki na Natasha.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...