Tuesday, March 1, 2016

MPOTO KUZINDUA VIDEO YA WIMBO SIZONJE JUMAMOSI, DAR

page
Muimbaji maarufu wa mashairi nchini, Mrisho  Mpoto Jumamosi Machi 5,  2016 atazindua video ya wimbo wake mpya Sizonje katika ukumbi wa Golden Jubilee  jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na mwandishi wetu, Mpoto alisema mgeni rasmi katika uzinduzi
huo atakuwa Mh. Waziri, wa Habari, Utamaduni, SanaanaMichezo Nape Nnauye.
mpoto-3.jpgMuimbaji maarufu wa mashairi nchini, Mrisho  Mpoto.
Alisema kuwa kabla ya uzinduzi huo kutakuwa na mjadala kuhusu
‘KufeliElimuSioKufeliMaisha’ ila kinachotakiwa ni kutokata tamaa. Ikiwa na
kauli mbiu ya INUKA ENDELEA.Alisema kuwa katika mjadala huo watu mbalimbali maarufu wakiwemo wasanii,
wanafunzi wa Vyuo Vikuu,  Wahadhiri pamoja na  wadau mbalimbali wa elimu
watazungumza kuhusu suala la elimu.
Mbali na watu hao pia wanatarajiwa kuwepo wanafunzi waliofanya vizuri zaidi
katika mitihani ya Kiswahili katika kidato cha nne pamoja na baadhi ya
wale, ambao hawakufanya vizuri ili kupata uzoefu wao na kujua ninikifanyike
ili kusonga mbele.

Aliwataja baadhi ya wasanii na watu wengine maarufu watakao zungumza siku
hiyo ni pamoja na Ruge Mutahaba, AY, Said Fella,  Niki wa Pili, Babu Tale,
George Kavishe, Miss Tanzania Lilian Kamazima, Mbunge wa MikumiP rofesa
Jay, Gardina, Shilole, Ommy Dimpoz na Mwana FA.

Alisema onesho hilo litafanyika katika ukumbi huo kuanzia saa 3:00 asubuhi.
Alisema kuwa video ya wimbo Sizonje ni elimu tosha ya Kiswahili, hivyo ni
muhimu mjadala wa Kiswahili ukafanyika siku hiyo yauzinduzi wake ili kuibua
mjadala wa kitaifa.

Alisema kuwa wanafunzi walio fanya vibaya katika mtihani wa kidato cha nne
mwaka jana ni wengi kuliko wale waliofaulu, hivyo ni muhimu kuwatia moyo
ili kuhakikisha hawakati tamaa na badala yake wanasonga mbele na
kuhakikisha wanafanya vizuri katika maisha.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...