Thursday, March 3, 2016

KHADIJA KOPA,MSAGA SUMU WAAHIDI KUFIA STEJINI TAMASHA LA AMSHA MAMA FESTIVAL KESHO!

Mkali wa miondoko ya Mipasho, Khadija Kopa (kushoto), akiongea na kujigamba jinsi alivyodhamiria kufanya makamuzi ya kufa mtu kwenye tamasha la Amsha Mama Festival katika viwanja vya Mwembe-Yanga, Temeke jijini Dar es Salaam kesho. Kulia ni Mratibu Mkuu wa tamsha hilo, Joe Kariuki, akimsikiliza kwa makini msanii huyo kwenye kikao cha waandishi wa habari kilichofanyika ndani ya Hoteli ya Travertine Magomeni jijini Dar es Salaam.
 Kopa, Msaga Sumu kupagawisha ‘Amsha Mama’ kesho
MKONGWE wa miondoko ya mipasho nchini, Khadija Kopa, na mkali wa Singeli, Msaga Sumu, hatimaye wamejitokeza na kujigamba kuwa kesho wataonyesha maajabu ya nguvu katika tamasha la Amsha Mama Festival litakalofanyika katika Viwanja vya Mwembe-Yanga Temeke jijini Dar es Salaam.

Wakizungumza mbele ya waandishi wa habari ndani ya ukumbi wa Travertine, Magomeni jijini Dar, Khadija Kopa na Msaga Sumu walisema kwamba kwa makamuzi waliyojipanga nayo kesho kwenye tamasha hilo kuna hatari ya ‘kufia jukwaani’ kwani wamejipanga kutoa burudani kwa wakazi wa Temeke kiasi ambacho hawajawahi kukifanya kwenye maisha yao.
“Kusema kweli sisi kwa pamoja tumejipanga kuwaburudisha mashabiki zetu wote kwani tuna uhakika kama tutapewa muda mrefu wa kufanya shoo basi kuna hatari ya kufia jukwaani kwani muziki wetu ni wa watu wa Temeke hivyo hatuna budi kesho kufanya kila linalowezekana ili tu tuweke historia mpya kupitia tamasha hili la Amsha Mama Festival”, alisema Kopa.
Kwa upande wa Mratibu Mkuu wa Tamasha hilo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa lebo ya Candy na Candy   Records, Joe Kariuki, tamasha hilo linalotarajiwa kufanyika mapema kesho ni mahususi kwa kuwaamsha wanawake wote wa Afrika Mashariki na Kati ili waweze kupata nafasi ya kujituma bila uoga katika biashara na kazi zao mbalimbali.

“Ukiachilia mbali hilo la kuwaamsha kinamama pia kesho kutakuwa na wasanii kibao wa hapa nchini wakitumbuiza, miongoni mwa wasanii hapo ni Juma Nature, Khadija Kopa, Mr Blue, Snura, Msaga Sumu, Ali Chocky, Roma, Young Killer na Tunda Man,” alisema Joe huku akiwataka watu wote wajitokeze kwa wingi kwani tamasha hilo ni la bure.

Mratibu Mkuu wa Tamasha hilo, Joe Kariuki, akisisitiza jambo juu ya tamasha hilo.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kikao hicho katikahoteli ya Travertine.
Mkali wa miondoko ya Singeli, Msaga Sumu, akielezea namna atakavyowapagawisha wakazi wa Temeke hiyo kesho.


No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...