Thursday, March 17, 2016

Kadja Nito adaiwa kuchumbiwa


KADJA NITO (5)
Staa wa Bongo fleva Khadija Maige ‘Kadja Nito’.
Mayasa Mariwata
MWANADADA anayefanya poa kwenye ulimwengu wa Bongo Fleva, Khadija Maige ‘Kadja Nito’ anadaiwa kuchumbiwa na kigogo mmoja (jina kapuni) hali inayomfanya kukaa kimya kimuziki.
Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika kilicho karibu na msanii huyo, bi’shosti huyo aliyekuwa akibamba na Wimbo wa Sina Maringo amekuwa akionekana viwanja mbalimbali akijiachia na kigogo huyo. “Sasa hivi mambo yake yamemnyokea, ndiyo maana siku chache zilizopita alionekana akila bata Sauzi, japo haonekani akipiga dili zozote zinazohusiana na kazi zake za kimuziki,” kilisema chanzo chetu.
Baada ya kunasa madai hayo, Showbiz Xtra ilimvutia waya Kadja kujua kama kuna ukweli ambapo alifunguka;“Hilo la kuchumbiwa siyo kweli jamani, ni kweli sionekani kupata dili za shoo hivi karibuni lakini siyo kwamba nimefichwa na mtu, hapana! Niwaambie tu mashabiki wangu, soon mtaona mambo makubwa kutoka kwangu sababu Sauz nilienda kikazi siyo kuuza sura kama wengi wanavyodhani.”

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...