Monday, October 5, 2015

IDD AZAN AITEKA KINONDONI

2
Idd Azan (katikati), akikatiza Mitaa ya Mkwajuni wakati akielekea kwenye mkutano wake wa kampeni  uliofanyika katika Kata ya Hananasifu, jana jioni.
3
Azan akiteta jambo na Hassan Dalali, mjumbe wa CCM, Kata ya Hananasifu.
45
Hassan Dalali akimkaribisha Azan kwenye kikao cha kampeni muda mfupi baada ya kuwasili mahali hapo.
6
Kikundi cha ‘kudansi’ kikitoa burudani mahali hapo.
7
Azan akinadi sera zake jukwaani  kwa wakazi wa Kata ya Hananasifu, Kinondoni jijini Dar es Salaam, jana jioni.
89,
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kinondoni, Idd Azan (katikati), akiwa amempakata mtoto aliyejitokeza na wazazi wake kusikiliza sera.
10
Mmoja wa wazee wa Kata ya Hananasifu akizungumza jambo na Azan baada ya kukutana naye njiani alipokuwa akielekea kwenye mkutano.
MGOMBEA wa kiti cha ubunge Jimbo la Kinondoni  kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),  Idd Azan jana aliwateka baadhi ya wakazi wa jimbo hilo waishio katika kata ya Hananasifu baada ya kukatiza kwa miguu wakati wa jioni alipokuwa akienda kwenye mkutano wa kampeni na baadhi ya wakazi wa kata hiyo kujitokeza kwa wingi na kuandamana naye hadi mahali mkutano ulipokuwa ukifanyikia.
Tukio hilo lilitokea majira ya saa 10:30 jioni ambapo Azan aliamua kutembea kwa miguu akitokea makao makuu ya ofisi za chama hicho zilizopo Kinondoni Mkwajuni jijini Dar es Salaam.
Habari/Picha: Musa Mateja/GPL

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...