WASTARA Juma Issa Abeid amekiri
kuzidiwa na hisia za kuwa na mwenza kutokana na ukweli kwamba damu yake
bado changa, hivyo suala la kuolewa halikwepeki huku akimpa nafasi kubwa
msanii mwenzake, Bond Bin Sinan endapo atakidhi vigezo na masharti.

Wastara Juma Issa Abeid akiwa na Bond.
Akifungulia ‘koki’ ya maneno mbele ya
paparazi wetu kwa njia ya simu mwanzoni mwa wiki hii, Wastara ambaye kwa
sasa yuko bize kusaka ubunge nyumbani kwao Morogoro Vijijini, alisema
hawezi kudanganya kwamba ataishi bila kuwa na mume kwa kuwa amekamilika
kimaumbile.
“Mimi ni mwanamke, nimekamilika tena
nakula na ninashiba. Damu bado changa. Nikisema siwezi kuolewa, nitakuwa
nadanganya. Nimekaa muda mrefu kwa sababu kila mwanaume anayenihitaji
ananitamani tu.
“Bond namuona ni mwelewa. Lakini nimempa
sharti la kutonigusa hadi siku ya ndoa. Kama atakidhi na hayo mengine
ambayo ni siri yetu, niko tayari kuolewa naye,” alisema Wastara.
No comments:
Post a Comment