Wednesday, July 8, 2015

MENEJA: KAJALA AMEPONA


Staa wa filamu Bongo, Kajala Masanja.
Gladness Mallya
MIEZI michache baada ya Kajala Masanja kugundulika kuwa na ugonjwa wa uvimbe kwenye kizazi, meneja wa msanii huyo, Leah Richard amesema hivi sasa yupo sawa kufuatia upasuaji wa mafanikio aliofanyiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
“Kajala kwa sasa yupo fiti na tatizo la uzazi limeisha, hivyo mashabiki wake wasiwe na wasiwasi kabisa kwani atarejea kazini kuendelea kuwapa burudani,” alisema meneja huyo baada ya simu ya msanii huyo kukosekana hewani.
Kajala, mmoja wa waigizaji wanaofanya vizuri katika Bongo Movie, alipatwa na wasiwasi baada ya kugunduliwa kwa uvimbe huo tumboni akihofu kutozaa tena, lakini kwa mujibu wa meneja wake, mafanikio hayo yamempa faraja kubwa na kumshukuru Mungu.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...