GOOD time! Ndivyo unavyoweza kusema ambapo wakati
habari ya mjini ikiwa ni kuhusiana na nyumba yake kupigwa mnada, staa wa
Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jaydee’ au ‘Jide’ yupo bize jijini
Hong Kong, China akila bata, Ijumaa Wikienda linakupa mchapo.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Kampuni ya Udalali ya MEM Auctioneers
and General Brokers ilipewa jukumu la kupiga mnada nyumba ya mwanamuziki
huyo iliyopo Mivumoni, Kinondoni jijini Dar baada ya Jide kushindwa
kulipa deni alilokopa kutoka taasisi ya fedha ya EFC Tanzania Limited.
Wanahabari wetu waliokuwa na kibarua cha kumtafuta Jide ili kujua
anazungumziaje kuhusu nyumba hiyo kupigwa mnada, walizunguka kwenye
viunga lukuki vya Dar ambavyo mwanamuziki huyo huwa anapatikana lakini
jitihada hazikuzaa matunda, achilia mbali simu yake ya mkononi
kutopatikana.
Wakati
gazeti hili likielekea mitamboni, chanzo kimoja kilipenyeza habari kuwa
staa huyo wa Wimbo wa Yahaya yupo nchini China ‘anakula ujana’.“Kwa
taarifa yenu Jide hayupo Bongo, ametimka zake China kula raha kama vipi
fuatilieni kwa mbinu zenu mtabaini hiki ninachowaeleza,” kilinyetisha
chanzo chetu, Jumamosi iliyopita.
Kabla ya kuwadadisi wadau wengine wa karibu wa Jide, Ijumaa Wikienda
liliingia kwenye ‘peji’ ya Instagram ya mwanamuziki huyo na kukutana na
posti iliyoonesha kuwa yupo Dubai akielekea nchini China kuinjoi maisha.
“Dubai-Hong Kong leo nimetoa ushamba sikujua mpaka ndege ikipaa kuna WiFi (huduma ya intaneti) tembea ujionee,” aliandika Jide.
Alipotafutwa Gardner G. Habash ambaye alikuwa mume wa Jide alisema
kwa kifupi kuwa hana taarifa zozote kuhusiana na nyumba hiyo kupigwa
mnada.
No comments:
Post a Comment