Tuesday, June 9, 2015

Mgogoro wa kimkataba kati ya Messi na Simba kitaeleweka leo…

MES
 
SHIRIKISHO la kandanda Tanzania, TFF leo linawakutanisha Simba na mshambuliaji wake, Ramadhan Singano ‘Messi’ kujadili utata wa mkataba uliopo baina ya pande hizo mbili.
Singano anadai ana mkataba wa miaka miwili aliosaini Mei mosi, 2013 na unatakiwa kumalizika Julai 1, 2015, wakati Simba inadai Messi ana mkataba wa miaka mitatu aliotia saini Mei 1, 2013 na unatakiwa kumalizika Julai 1, 2016.
Kutokana na utata huo, inaonekana kuna upande umechakachua mkataba na leo kinaweza kueleweka.
Juni 5 mwaka huu, TFF ilitangaza kumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za mgogoro wa kimkataba kati ya Mchezaji Ramadhani Singano na klabu ya Simba.
TFF ikaagiza mwakilishi wa klabu ya Simba pamoja na mchezaji wa Ramadhani Singano wafike ofisi za TFF siku ya Jumanne tarehe 09/06/2015 kwa mazungumzo na Kila upande umetakiwa kwenda na vielelezo vyake.
“Katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye mazungumzo,TFF inaziasa pande zote mbili zijiepushe na kutoa matamko yanayoweza kuchochea hali ya kutoelewana na kuamsha hisia mbaya katika familia ya mpira wa Miguu Tanzania”. Alisema sehemu ya taarifa ya TFF.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...