Monday, June 8, 2015

IMEFICHUKA: JOKATE ATAKA KUJIUA!

Brighton Masalu
Imefichuka! Sexy lady mtafutaji anayejishughulisha na fani lukuki ikiwemo urembo na muziki, Jokate Urban Mwegelo ‘Kidoti’ kwa mara ya kwanza ameweka wazi kwamba alitaka kunywa sumu kisa kikiwa ni kuumizwa kimapenzi na mwanaume aliyempenda kupindukia, aya zifuatazo zimesheheni.
Sexy lady mtafutaji anayejishughulisha na fani lukuki ikiwemo urembo na muziki, Jokate Urban Mwegelo ‘Kidoti’,
MBELE YA GAZETI HILI
Akizungumza katika spesho intavyu na gazeti namba moja la mastaa Bongo, Ijumaa Wikienda, wikiendi iliyopita, Jokate au Jojo alifunguka kwamba, japokuwa haikujulikana kwa watu wa nje kutokana na usiri mkubwa uliofanywa na ndugu zake, akiwemo mama mzazi, lakini ameona ni vyema akaweka wazi ili watu wajifunze namna ambavyo mapenzi yanaweza kuharibu mustakabali mzima wa maisha ya mtu.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
KWANI JOKATE ALIWAHI KUTOKA NA NANI?
Jokate ambaye amewahi kutajwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mastaa mbalimbali Bongo wakiwemo staa wa mpira wa kikapu ambaye ni Mbongo anayekipiga nchini Marekani, Hasheem Thabeet Manka, wanamuziki, Ali Saleh Kiba, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Mtangazaji Millard Ayo wa Clouds FM, alisema hakuona sababu ya kuendelea kuishi bila mwanaume huyo na kuona njia pekee ni kujitoa uhai!
Hasheem Thabeet Manka katika pozi na Jokate.
AKIRI KUJIFUNGIA NDANI
Katika mahojiano hayo yaliyochukua takriban dakika 30, Jokate alikiri kujifungia ndani mara kwa mara na kujaribu kunywa sumu lakini alikuwa akishtukiwa na ndugu zake hivyo kushindwa kutekeleza zoezi  hilo.
Jokate akiwa katika pozi na Millard Ayo.
USHAURI WA KISAIKOLOJIA
Alisema kufuatia hali hiyo, ilibidi awe chini ya uangalizi maalum, huku akiwa anaishi kama mfungwa na mara nyingi akipewa ushauri wa kisaikolojia na baadaye kujikuta akimfuta mwanaume huyo moyoni.
Staa wa Bongo fleva, Ali Kiba.
“Wewe acha tu, hakuna kitu kinachouma kama mapenzi, niliumia mno, ilikuwa mbaya mno kwangu kwani nilitaka kujiua baada ya kuona kabisa siwezi kuishi bila huyo mwanaume kwa sababu nilimpenda sana tena sana.
 KHA! AJARIBU KUNYWA SUMU!
“Nilijaribu kunywa sumu mara kadhaa lakini nilikuwa naokolewa na ndugu zangu, nashukuru nilipewa uangalizi maalum kutoka kwa ndugu.
“Unajua ukiniona huwezi kujua kama huwa naumizwa na mapenzi kwa sababu mimi ni msiri sana kwa mambo yangu binafsi kama hayo,” alisema Jokate akionekana ni mtu ambaye akipenda huwa anapenda kweli na kuongeza:
Jokate Mwegelo.
“Lakini baadaye nilitafutiwa mtaalam wa saikolojia, akanipa ushauri, nikajikuta nimemuondoa kabisa huyo mtu moyoni mwangu, nikaelekeza nguvu zote kwenye kazi zangu za mitindo kupitia nembo yangu ya Kidoti.”
Ijumaa Wikienda: Je, ni Millard Ayo?
Jokate: Hapana lakini Millard ni mtu ambaye napenda anavyojituma kwenye kazi yake ndiyo maana ni mtu wangu wa karibu.
Ijumaa Wikienda: Je, Ni Diamond?
Jokate: Oooh…nooo!
Ijumaa Wikienda: Basi atakuwa ni Kiba au?
Jokate: Hapana, Kiba ni mtu wangu wa kikazi, napenda kuwa naye karibu kwani najifunza vitu vingi kwake kuhusu muziki.
Ijumaa Wikienda: Au ni Hasheem Thabeet?
Jokate: Teh…Tehee…Teheee…Ijumaa Wikienda bwana!
Ijumaa Wikienda: Basi acha tujiongeze.
Jokate: Ndiyo jiongezeni lakini ni kweli siwezi kumsahau maana aliniachia msiba mzito moyoni.

TUJIKUMBUSHE
Jokate na Hasheem waliwahi kuripotiwa kuwa katika uhusiano ‘siriaz’ huku minong’ono ya kufunga ndoa ikisambaa lakini ghafla shetani alikunjua makucha na kuikwaruza mipango hiyo huku Hasheem akituhumiwa kuibuka Bongo na mtoto ‘shombeshombe beibi’ kutoka ardhi ya Rais Barack Obama.
 Kujua mengi zaidi tembelea www.globaltvtz.com

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...