Wednesday, May 13, 2015

VITUKO BABY SHOWER YA AUNT EZEKIEL


Wasanii wawili mahasimu katika tasnia ya filamu, Kajala Masanja (kulia) akiwa kamkumbatia rafiki yake Aunt Ezekiel, usiku wa kuamkia Mei 10, mwaka huu katika Viwanja vya Ndoto Polepole, huko Bagamoyo mkoani Pwani.
Kajala akiweka sawa nywele zake.
Keki iliyoandaliwa kwenye sherehe hiyo.
Aunt Ezekiel akikata keki hiyo.
Aunt Ezekiel akimlisha keki mpenzi wake, Moze Iyobo.
...Wakifanya yao.
Moze Iyobo akishika tumbo la mpenzi wake huku wakiwa wamekumbatiana.

Marafiki na ndugu waliofika katika sherehe hizo.
Kajala Masanja akitembea kwa pozi.
Marafiki zake na Aunt wakicheza.
Kajala Masanja (mwenye nguo nyekundu) akicheza muziki.
....Akizidi kuonyesha ufundi wa kucheza.
Akiwa na mashost zake.
Warembo wakiwa katika pozi mbalimbali.
Wakiwa katioka picha ya pamoja na Aunt Ezekiel.
(PICHA: MUSA MATEJA/GPL)
Waandishi wetu VITUKO kibao vilitawala juzikati kwenye sherehe ya ujio wa mtoto wa staa wa filamu Bongo, Aunt Ezekiel  (Baby Shower), baada ya mastaa na waalikwa kibao kuonekana kufanya vituko vya hapa na pale.
Tukio hilo lilijiri usiku wa kuamkia Mei 10, mwaka huu katika Viwanja vya Ndoto Polepole, huko Bagamoyo mkoani Pwani, ambako waalikwa walipata fursa ya kula, kucheza na baadaye kutoa zawadi kwa ajili ya mtoto atakayezaliwa.
Aunt Ezekiel alimtambulisha mpenzi wake, Moze Iyobo kwa kumlisha keki kabla ya kumwagiana mabusu na kunyonyana ndimi hadharani.

Licha ya tukio hilo, pia waalikwa walicheza vyema muziki kwa shangwe na furaha huku wakizungusha nyonga kwa ustadi wa aina yake.Waalikwa waliokuwa wamevalia sare za aina mbili, walikuwa burudani ya aina yake huku karibu wote, wakienda kulibusu tumbo la Aunt ambalo sasa limekuwa kubwa kiasi cha kuonekana kuwa ni mtu wa kujifungua leo au kesho.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Aunt alisema anashukuru marafiki na ndugu zake kwa kuwezesha shughuli hiyo kufanyika, kwani awali aliamua aifanye baada ya mtoto wake kuzaliwa.“Nimefurahi sana maana watu wamejitolea kwa hali na mali na kubwa zaidi ni hii sehemu ambayo tumefanyia sherehe, kiukweli ni mbali sana hivyo inanifanya kuamini kila aliyeweza kuja huku ana mapenzi ya dhati na mimi,” alisema Aunt.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...