Friday, May 8, 2015

STOP!! OMMY DIMPOZ MARUFU NYUMBANI KWA DIAMOND                      DSC02277    

*Alianza usnichi tangu mwaka jana lakini safari hii kapiliza
*Hatakiwi kuonekana hata mtaani kwa Diamond

Mkali wa wimbo wa Wanjera Omari Nyembo a.k.a Ommy Dimpoz hatakiwi kuonekana kwenye makazi (state house) ya Mwanamuziki tajiri nchini Nasibu Abdul’, maarufu Diamond Platinumz kuanzia sasa!

Habari toka vyanzo vya kuaminika zinasema kuwa urafiki wa Ommy Dimpoz na Diamond uliingia doa tangu mwaka jana huku chanzo kikielewa kuwa ni tabia ya Ommy Dimpoz kutaka kuiga kila kitu anachofanya Dimond  na wakati mwingine kujifanya yeye ni zaidi ya mwanamuziki huyo.
Kutokana na tabia hiyo ndipo Diamond akaanza kumtenga Dimpoz taratibu lakini mambo yalikuja kuharibika zaidi baada ya Ommy Dimpoz kumtunishia kifua Diamond kwa kujenga urafiki na ex-girlfriend wake Wema Sepetu huku akiachia picha za ajabuajabu alizopiga na Wema katika Mitandao ya Kijamii.

“Unajua Diamond amemsaidia sana Dimpoz kujulikana kimuziki hivyo alipaswa kumheshimu hata kama kamkosea, sasa Dimpoz baada ya kuona ametoka kimuziki akaanza kutaka kuishi kama Diamond,wakati mwingine akawa anajifanya yupo juu kuliko Diamond ndipo Diam0nd akaanza kumtenga taratibu.

“Lakini badala ya kujirekebisha akaanza kutanua kifua zaidi kwani alipokuja kusikia Diamond na Wema wameachana na haziivi yeye akajiweka kwa Wema na kuanza kutengeneza mazingira ya kujionesha  kwa watu kuwa Wema ni demu wake!.   
CHANZO: GAZETI LA KIU

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...