Brighton Masalu na Musa Mateja
SIKU
chache baada ya kuripotiwa na gazeti pacha la hili, Risasi Jumamosi
kuwa staa wa sinema za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’ alibeba mimba
na kuzaa kwa siri huku tetesi zikivuma kuwa baba wa mtoto huyo ni msanii
mwenzake, Vincent Kigosi ‘Ray’, mambo yameanza kunoga baada ya Ray
kufunguka kuwa hahusiki kwa lolote, Risasi Mchanganyiko ‘limemzingira’.
Hivi karibuni gazeti hili lilimbana staa huyo anayetamba sokoni kwa
sasa na Filamu ya Chicken Head baada ya kubambwa nje ya Ukumbi wa
Mwalimu Nyerere, Posta jijini Dar, kulikokuwa na sherehe za Tuzo za TAFA
ambapo aliweka wazi.
Awali, Ray alisema si busara wala hataki...
kuzungumza mengi juu ya madai hayo kwani hahusiki kwa lolote na
kwamba watu wasimtafsiri kutokana na maneno yasiyokuwa na ukweli huku
akimtaja mpenzi wake wa sasa, Chuchu Hans kuwa ndiye mwanamke wake wa
maisha.
Ray alifunguka kuwa, kati ya mambo yanayomchukiza ni ama
kuzushiwa au kuhusishwa na mambo ambayo yanamfanya aonekane wa hovyo
katika jamii na kusisitiza kusiwepo na mjadala unaopingana na kauli
zake.
Huku akiwa amemganda Chuchu kimahaba mbele ya kadamnasi, Ray
alikwenda mbele zaidi na kusema ni jambo la heri kujiweka mbali na watu
wanaotafuta umaarufu kupitia migongo ya watu, kauli iliyozua viulizo kwa
waandishi wetu na yeye kushindwa kuifafanua kwa kile alichokiita
‘hakuwa na mudi ya mazungumzo zaidi’.
“Achaneni na hayo mambo, sihusiki kwa lolote na jambo hilo (mtoto) na
sipendi kabisa kuzushiwa mambo kama hayo, watu wasinitafsiri kwa
minong’ono na badala yake wafuate ninachokisema.
“Kwa sasa mwanamke wa maisha yangu ni huyu (Chuchu) na nitakuwa
natembea naye kila mahali ili kuwafunga midomo wanaojinadi kuwa ni
wapenzi wangu,” alisema Ray huku akiwatazama waandishi wetu kwa macho ya
‘nadhani mmenielewa sasa’ na kuondoka eneo hilo sanjari na mahabuba
wake.
Hivi
karibuni Johari alithibitisha kuwa na mtoto wa kike mwenye umri wa
miezi saba ambaye alimpa jina la Maria linalofanana na la mama wa Ray
hivyo kuibua minong’ono kuwa huenda jamaa huyo anahusika.
No comments:
Post a Comment