Saturday, May 2, 2015

MAYWEATHER VS PACQUIAO NANI BINGWA?


Mayweather na Pacquiao wakitambiana.
Japo tayari ni tajiri, Mayweather ambaye jina lake la utani ni Money, atapokea zaidi ya dola milioni 150 na Pacquiao kama dola milioni 100.Ni Mayweather au Pacquiao Las Vegas? Pacquiao yeye ametoka jamii ya kimaskini huko Ufilipino na kuna wakati katika maisha yake ya utotoni aliwahi kulala njaa.
Floyd Mayweather akipima uzito.
Achilia mbali wanaoangalia kwenye TV, wengi wa mashabiki  huko Marekani wangependa kuona makonde yakirushwa 'LIVE' hivyo wamekubali kutoa ada ya hadi dola milioni 100 kwa kichwa kushuhudia wakiwa 'LIVE' nje ya ulingo.
Wenye uchu wa kushuhudia pambano hilo 'LIVE' lakini hawajapata tiketi wako tayari kuzipata kwa walionanazo huku dau likiwa limepandishwa kwa kiwango atakacho muuzaji huyo mchuuzi.
Wafilipino kumshangilia Pacquiao
Wakati huohuo wito umetolewa kwa wakazi wa kisiwa kimoja cha Philippines kwamba watumie umeme kwa kiasi kidogo ili kumwangalia katika runinga zao hapo Jumapili shujaa wao Mfilipino mwenzao , Manny Pacquiao (36) atakapokuwa akipambana na Mmarekani Floyd Mayweather (38) kwenye ulingo wa shindano la ndondi linalotajwa kuwa kubwa zaidi siku za hivi karibuni.
Manny Pacquiao akipima uzito.
Wakazi hao wameshauriwa na kampuni ya umeme nchini humo Palawan kuzima vifaa vinavyotumia umeme majumbani kama friji, mashine za kufua nguo na pasi ili kuhifadhi umeme kwa ajili ya  kuwashia runinga zao.
Ushauri huo umetolewa kwani kisiwa hicho hukumbwa na upungufu wa umeme mara kwa mara, hivyo ni sharti wafuate maagizo hayo ili wasikose kushuhudia na kumshangilia kinara wao huyo atakayeshiriki pambano hilo litakalofanyika huko Las Vegas Jumamosi usiku saa za Marekani.
Ndilo pambano lililovutia fedha zaidi kuwahi kutokea.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...