Thursday, May 28, 2015

JOKATE: ALI KIBA NI KILA KITU KWANGU

Na Musa Mateja
MREMBO mchakarikaji Bongo,  Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, juzikati aliamua kuvunja ukimya na kusema kuwa mwanamuziki Ali Kiba kwa sasa ndiye kila kitu katika mambo yake mengi ya kimaisha.

Mrembo mchakarikaji Bongo,  Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.
Akizungumza na Ijumaa Jokate alisema, watu wanaongea sana kuhusiana na ukaribu wao bila kujua kuwa Kiba ni mtu wake kitambo na sasa ndiye kila kitu kwake kwani ana projekti naye kibao ambazo zinakuja na wasioelewa, ipo siku wataelewa.
Mwanamuziki Ali Kiba.
“Yaani watu wangu wajue Kiba ni kila kitu kwangu ila siyo ishu ya mapenzi, tuna projekti kibao, nawaomba watu wavute subi--ra watajionea kila kinachoendelea kati yetu.Kuanzia sasa Kiba atakuwa akipeperusha ‘brand’ za Kidoti kwa kila atakachofanya ikiwa ni pamoja na mavazi,” alisema Jokate.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...