Friday, May 22, 2015

JINI KABULA & SHERMAN PROJECT YA MAHABA MAZITO Muigizaji wa Bongo Muvi, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula.

Straika wa Yanga, Kpah Sherman.

Nicodemus Jonas na
Musa Mateja

LICHA ya kuwa na muda mfupi tangu atue nchini kucheza soka akitokea nchini Cyprus, straika wa Yanga, Kpah Sherman amekuwa akiandamwa na matukio ya ajabu.

Awali alipoanza kazi alionyesha uwezo wa juu katika mechi dhidi ya Simba ya Mtani Jembe lakini hakumaliza mchezo huo, aliumia na kutolewa.
Baada ya hapo akapewa mkataba, kilichofuata ni kuwa hakuonyesha uwezo wa juu kama ilivyotegemewa licha ya kupewa nafasi na kocha wake, Hans van Der Pluijm.
Baadaye akakutana na tukio la kuibiwa mali zake zilizokuwa chumbani katika nyumba aliyokuwa akiishi maeneo ya Sinza-Shekilango jijini Dar inadaiwa aliibiwa na ‘kiburudisho’.
 Hapo katikati akazama kwenye penzi la muigizaji wa Bongo Muvi, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’, baada ya kudumu kwa muda mfupi, ‘wakamwagana’.
Siku chache baada ya kutengana, Kabula akaibuka katika mitandao ya kijamii na kushusha lugha kali kwa Sherman huku akiweka picha ya mchezaji huyo akiwa kitandani.
Kama filamu vile, siku chache baada ya Kabula kuwasha moto huo, kukaibuka picha zinazomuonyesha Kabula akiwa mtupu akioga. Gazeti hili lilizungumza na wahusika wote kwa nyakati tofauti.
Championi: Kabula unamjua Sherman?
Kabula: Ndiyo namjua, alikuwa mtu wangu lakini siyo kwa sasa, kila mtu yuko kivyake.
Kwa nini ulimtusi kwenye mtandao?
Kabula: Alinitibua na mimi nikaamua kumtusi kupitia Insta.
Unahisi yeye ndiye amehusika na picha zako za utupu?
Kabula: Nashindwa hata nikueleze vipi, sababu kichwa changu nakisikia hakiko vizuri. Sina namna ya kuzielezea picha hizo, kama ni kudhalilika nimeshadhalilika sana, maana kama ni kusambaa kwenye mitandao zimesambaa na kila mmoja anaongea kivyake.
Hata nikitaka nilifafanue naona nitazidi kusababisha makubwa na kuwachongea wengi. Kwa kuwa limeshatokea basi namuachia Mungu, naamini nalo litapita na maisha yataendelea, lakini suala la hizo picha sitaki kumtuhumu moja kwa moja.
Upande wa Sherman ambaye ni raia wa Liberia mahojiano yalikuwa hivi:
Una uhusiano gani na Kabula?
Sherman: Kabula alikuwa mpenzi wangu lakini hatukudumu sana, kwa kuwa nilipata taarifa zake mbaya nikaamua kujiweka kando. Amekuwa akinitafuta ila simtaki na sitaki kumuona.
Kuna picha zake za utupu zimesambaa, unahusika kwa chochote?
Sherman: (Anacheka) Labda akili hazimtoshi, mimi siwezi kufanya upuuzi kama huo. Aseme kweli kama anatafuta ‘kick’ kwangu ijulikane.
Nitakuwa mjinga gani wa kuweka upuuzi wa namna hiyo kwenye mtandao, ndiyo maana niliamua kuachana naye baada ya kuambiwa tabia zake chafu.
Kabla ya Kabula uliwahi kuwa na uhusiano na staa yeyote?
Sherman: Hapana na sitaki kuwasikia tena.
Lakini kuhusu…
Sherman: (Anamkatisha mwandishi) Hakuna kitu kama hicho (Inadaiwa kuwa aliwahi kuwa ‘karibu’ na Dokii na Snura).

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...