Saturday, May 30, 2015

CHIKOKA ANASWA NA ‘KIBURUDISHO’

 
Msanii wa filamu category ya ‘siriaz komedi’, Juma Chikoka ‘Chopa’ akiwa na dada huyo.
Brighton Masalu MSANII wa filamu category ya ‘siriaz komedi’, Juma Chikoka ‘Chopa’ amenaswa ‘laivu’ akiwa na mrembo huku akionesha hali ya kutojiamini na kutoa tafsiri hasi miongoni mwa baadhi ya watu.
Mwanahabari wetu alimnasa msanii huyo mwishoni mwa wiki iliyopita ndani ya Jengo la Mwalimu Nyerere, Posta jijini Dar,  kulikokuwa na sherehe za utoaji Tuzo za TAFA huku akimchimba mkwara mwandishi wetu akimtaka kusitisha zoezi la ‘kuwafotoa’ picha.
Awali, mwandishi wetu alimshuhudia Chikoka akiingia ukumbini humo na kuketi mkao wa ‘ kusikiliza misa’ kabla mrembo huyo hajatinga ndani na kumfanya msanii huyo asahau ghafla maana ya msamiati utulivu jambo lililowafanya baadhi ya watu kugeuza shingo mara kwa mara kuwatazama.“Oyaa, achana na mambo ya picha bwana hebu tupe uhuru wa kufurahia kilichotuleta hapa,” alisema Chikoka.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...