MCHEZA filamu anayefanya vizuri nchini, Isabela
Francis ‘Vai’ amefunguka na kuchekelea kuachana na mpenzi wake
ajulikanaye kwa jina la Boniface Matiku ‘Bonny’, akisema akiwa nyumbani
kwa mama yake, ana uhuru wa kuamua chochote, ikiwa ni pamoja na kunywa
pombe hata asubuhi.
Akizungumza na Risasi Mchanganyiko hivi karibuni, Vai alisema
zilipendwa wake huyo amekuwa akimuomba msamaha na kudai atamrudishia
fedha za televisheni aliyoweka dhamana, lakini hataki kwani nyumbani
kwao anaona raha kutokana uhuru alionao.
“Nyumbani ni raha sana, kwani nikitaka kulewa nalewa hata asubuhi,
niko huru zaidi ya nilivyokuwa kwa Bonny, hivyo sina mpango wa kurudiana
naye kwa sasa japokuwa ananiomba msamaha sana lakini sitaki, ngoja
nipumzike kwanza kwa mama yangu,” alisema Vai.

No comments:
Post a Comment