Wednesday, April 8, 2015

NAY, SHAMSA WADAIWA KUPIKA NA KUPAKUA
Musa Mateja
KILICHOJIFICHA nyuma ya pazia la uhusiano wa mastaa wa Bongo, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’, na Shamsa Ford sasa kimevuja baada ya Risasi Mchanganyiko kunasa habari za wawili hao kuwa kwenye uhusiano wa mapenzi kiasi cha kudaiwa kupika na kupakua pamoja.
Staa wa Bongo fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.
Chanzo makini kimeeleza kwamba, wawili hao ambao kila mmoja katika siku za hivi karibuni aligombana na mwenza wake wa awali, wamekuwa katika uhusiano wa kimapenzi kwa uficho wa hali ya juu, wakionekana mara kwa mara nyumbani kwa Mbongo Fleva anayeishi Kimara Korogwe, jijini Dar.
Inadaiwa kuwa kwa zaidi ya wiki tatu sasa wawili hao wamekuwa wakionekana katika gari moja, wakitoka au kuingia nyumbani kwa Nay wakitokea mjini kwenye mihangaiko yao ya kila siku.
“Kama ulikuwa hujui vizuri naomba nikujuze, Nay na Shamsa wanaonekana walikuwa wakifuatiliana kwa muda mrefu, nasema hivi kwa vile siku chache tu baada ya wawili hawa kuachana na watu wao wa zamani, leo wako pamoja tena wanaonyeshana mahaba utadhani walikuwa pamoja miaka mia iliyopita,” alisema mtoa habari wetu.
 
Staa wa bongo muvi, Shamsa Ford.
Ili kuthibitisha maneno yake, chanzo chetu kilituma picha kadhaa za wawili hao wakiwa nyumbani kwa Nay, huku akisisitiza kuwa hata dada na ndugu wa mwanaume huyo, nao wamekuwa wakipost picha za Shamsa ambaye hivi sasa anapika na kupakua nyumbani kwa mkali huyo wa kibao cha Nakula Ujana.

Chanzo kilimtafuta mkali wa filamu Shamsa Ford ili azungumzie suala hilo, ambaye hata hivyo, alichengachenga kabla ya kusema kuwa ukaribu baina yao, unatokana na ‘bonge la project’ ambayo itakuwa mitaani ‘soon’.
Kwa upande wake, Nay wa Mitego alipoulizwa kuhusu ukaribu huo, alisema hadhani kama ni jambo la haki kwake kuulizwa kuhusu suala hilo, wakati inajulikana kuwa yupo ‘single’.
“ Bwana eeh mimi na Shamsa ni wasanii halafu ukiachia mbali hilo kuwa karibu naye si tatizo wala sioni cha ajabu maana yeye yupo single na mimi nipo single labda kama kuna kipya hapo unaweza kuniambia nikakuelewa, ila ishu ya kuja kwangu au mimi kuwa kwake sioni kama ni ishu,” alisema.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...