Tuesday, April 7, 2015

BABA YAKE MKUDE AZIKWA KINONDONI JIJINI DAR

  Mkude akiwa ameshikilia msalaba wa baba yake katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar leo jioni.
Mkude akiweka shada la maua baada ya mazishi ya baba yake katika Makaburi ya Kinondoni, Dar.
Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ akiweka shada ya maua katika kaburi la mzee Gerald Mkude ambaye ni baba mzazi wa kiungo wa Simba, Jonas Mkude, leo jijini Dar.
 MZEE Gerald Jonas Mkude ambaye ni baba mzazi wa kiungo mkabaji wa Simba, Jonas Mkude amezikwa leo Jumanne jioni katika Makaburi ya Kinondoni jijini Dar, baada ya kusumbuliwa na matatizo ya figo tangu Novemba mwaka jana.

Mzee huyo ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 46, alilazwa katika Hospitali ya Mwananyamala tangu Alhamisi ya wiki iliyopita kabla ya Jumapili kufariki akiwa katika hospitali hiyo ya Mkoa wa Kitabibu wa Kinondoni.
Bwana ametoa na bwana ametwaa na jina lihimidiwe, amina.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...