Tuesday, March 3, 2015

TFF YACHEFUA HALI YA HEWA KUMRUHUSU AJIBU KUIVAA YANGA.

Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ya kumruhusu straika wa Simba, Ibrahim Ajib kuruhusiwa kucheza mchezo wa Jumapili dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga, imezua tafrani kufuatia wadau wa soka kulijadili kwa kina na kushindwa kuelewa ni aina gani ya sheria iliyotumika kumruhusu.

Imebainika kuwa Ajibu ameruhusiwa kucheza mchezo wa Jumapili kwa kutumia kipengele cha kanuni No 75 kinachoeleza kuwa kamati inaweza kufanya mabadiliko katika vipengele vya katiba yake, lakini barua iliyotumwa kwa Simba na nakala kwa klabu husika, inaoneshwa kuwa tayari kanuni hizo zimeishafanyiwa mabadiliko. Jambo ambalo linaleta utata.
Kanuni ya Bodi ya Ligi No 37 kifungu no 4 kinajieleza kama kilivyo kwenye 'attached' hapa chini.
Ally Sulu ambaye ni kiongozi wa kamati ya Simba, ndiye alipost kipengele kinachomruhusu Ajibu kucheza mchezo na Yanga.
Habari za chinichini zinasema kuwa Yanga wanaweza kumgomea mchezaji huyo kucheza Jumapili lakini bado hazijathibitshwa.
Ajibu ambaye wikiendi iliyopita alipiga hat trick ikiwa ni ya kwanza msimu huu wakati Simba ikiishindilia Tanzania Prisons mabao 5-0, anakabiliwa na adhabu ya kukosa mchezo mmoja kutokana na kuwa na kadi tatu za njano katika michezo mfululizo, lakini TFF imewapa 'option' Simba kuchagua mchezo ambao wangependa mchezaji huyo akose, na kumuamulia kuikosa Mtibwa Sugar.
Adhabu yake ilikuwa ianze katika mchezo dhidi ya Prisons wikiendi iliyopita lakini akacheza kwa ruhusa ya TF.
TFF imefunguka kuwa ilifanya mabadiliko hayo mwezi Feburuari mwaka huu, lakini baadhi ya klabu zimekataa kuwa hazina taarifa na mabadiliko hayo.

Barua kutoka kwa Bodi ya Ligi ya kumsafisha Ajibu kuwa huru kuwakabili Yanga Jumapili wikiendi hii.
Ajibu anakabiriwa na kipengele cha nne katika kanuni za TFF kupitia wasimamizi wakuu wa ligi- Bodi ya Ligi

Picha iliyopostiwa na mjumbe wa kamati tendaji ya Simba, Ally Sulu akieleza kipengele kinachomlinda Ajibu kuwa ni No. 75 ya kanuni hizi. Sulu alipost Facebook akijiteta wanadau waliopinga maamuzi ya TFF katika hili.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...