Friday, March 6, 2015

SIMBA YAONGEZA WATENDAJI WENGINE BENCHI LA UFUNDI

Simba  katika moja ya mazoezi.
Kikosi cha madaktari wanne wa kitengo maalum cha kuchua misuli kutoka katika Kituo cha Afya cha Malindi mjini hapa, wametua kwenye kambi ya Simba iliyopo Chukwani kwa ajili ya kazi maalum ya kuwachua misuli wachezaji wa timu hiyo na huduma nyingine zitakazohitajika.
Madaktari hao walipelekwa kwenye kambi hiyo ambapo wachezaji wamekuwa wakijifua kujiandaa na mechi dhidi ya Yanga itakayopigwa keshokutwa Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Akizungumzia ujio wa madaktari hao, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Abdul Mshagama ambaye makazi yake yapo kisiwani hapa, alisema madaktari hao walipelekwa kambini kutokana na aina ya mazoezi wanayofanya wachezaji pamoja na umuhimu wa mechi husika.
Akiwazungumzia madaktari hao, Daktari wa Simba, Yasin Gembe, alikiri kufanya kazi na madaktari hao lakini alisema hawezi kuongelea zaidi suala hilo kwa kuwa hayo ni masuala ya ndani ya kambi, hivyo si vizuri kuweka wazi kila kitu.

“Ni kweli niko na madaktari hao lakini siwezi kuliongelea zaidi suala hilo kwa kuwa hayo ni mambo ndani ya kambi,” alisema Gembe.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...