Tuesday, March 3, 2015

PAM D: SIMTEGEMEI MESEN KWENYE MUZIKI

Mwanadada mtangazaji na mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini, Pamela Daffa ‘Pam D’.
Shani Ramadhani
LEO tunaye mwanadada mtangazaji na mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini, Pamela Daffa ‘Pam D’ ambapo ameweka wazi kuwa mbali na undugu alionao na Mesen Selekta kila mtu anafanya kazi kivyake yaani yeye ni muandishi wa mistari, Mesen ni prodyuza na mwanamuziki.

Akihojiwa na safu hii, huku akirekodiwa na ‘kruu’ ya Global TV Online mwishoni mwa wiki iliyopita katika Chumba cha Habari cha Global Publishers, Pam D alisema mbali na kuwa muimbaji na mtangazaji yeye ni muigizaji na densa, ifuatayo ni sehemu ya mahojiano ambayo pia unaweza kuyapata kupitia tovuti ya www.globaltvtz.com ;

Pamela Daffa ‘Pam D’.
Mwandishi: Ni lini kipaji chako cha kuimba kilianza kuonekana?
Pam D: Kama kuanza sijaanza leo lakini rasmi nimeanza mwaka jana na ngoma yangu ya Nimempata ambayo nimeshirikiana na Mesen Selekta.
Mwandishi: Kwa mara ya kwanza kabisa wewe kuanza kuimba ulianza na wimbo upi?
Pam D: Niliimba wimbo ambao nilikuwa nimeshirikiana na Darasa kupitia Studio za Classic Sound chini ya Mona Gangstar lakini kipindi chote hicho sikuwa siriazi na wala sikujua watu wananichukuliaje lakini sasa hivi nimekuja rasmi.
Mwandishi: Wengi wanasema kwamba Mesen anakuinua sana kwenye muziki wako kuanzia kwenye utunzi wa mistari mpaka kukuandalia, ikoje hiyo?
Pam D:  Ifahamike tu kwamba hata kama Mesen ni ndugu yangu lakini familia yetu sisi karibu wote ni wanamuziki na kwenye kazi kila mtu anafanya yake, mimi naandika mwenyewe na yeye ni prodyuza.
Mwandishi: Unazungumziaje soko la muziki wa Bongo Fleva sasa hivi?
Pam D: Kwa sababu nimeanza nashukuru Mungu napata mialiko sehemu mbalimbali na karibu kila siku napigiwa simu na kuambiwa wimbo wangu unafanya vizuri na muziki unalipa.
Mwandishi: Mbali na Mesen Selekta ni maprodyuza gani wengine unawakubali?
Pam D: Nawaelewa maprodyuza wote ambao wanafanya vizuri, wapo wengi sana kama Master J, Marco Chali, Mona Gangstar, Duke na wengine wengi.
Mwandishi: Unawazungumziaje wasanii ambao wanakimbilia kurekodi nje na ni kweli maprodyuza waliopo hapa hawajui kutumia vifaa?
Pam D: Msanii kama msanii ni lazima aangalie soko la muziki linakwendaje ndiyo maana wanaangalia sehemu ambayo wao wanaona inawatoa na wanaweza kufanya vizuri na jamii ikawakubali na inasemekana kuwa ile ni njia mojawapo ya kuwafanya wasanii wajulikane kimataifa.
Mwandishi: Vipi unapata usumbufu gani kwa wanaume hasa mastaa?
Pam D:  Sijaona kama kuna usumbufu sana kwa sababu usumbufu ni jinsi ambavyo mwenyewe unajiweka lakini kama ninajiheshimu na ninajiamini siwezi pata.
Mwandishi: Mbali na utangazaji na uimbaji una fani gani nyingine?
Pam D: Nina vipaji vingi sana ambavyo sijavifanyia kazi, ni densa na pia najua kuigiza.
Mwandishi: Baada ya Nimempata unawaambia nini mashabiki wako?
Pam D: Nawapenda sana na nawashukuru kwa kunifagilia kwamba wimbo wangu unafanya vizuri, hivyo wakae mkao wa kula kusubiri kibao changu kipya ambacho nitamshirikisha Christian Bella ‘Mfalme wa Masauti’.
Mwandishi: Una mpenzi? Na je unapenda kuwa na mwanaume mwenye sifa zipi?
Pam D: Nampenda mwanaume mwenye mapenzi ya dhati kwangu, anayejali, atakayeheshimu kile ambacho mimi ninakifanya na awe tayari kwa chochote juu yangu.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...