Tuesday, March 10, 2015

MKE WA GBAGBO AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 20 JELA


Simone Gbagbo aliyekuwa mke wa Rais wa Ivory Coast, Laurent Gbagbo.
MAHAKAMA moja nchini Ivory Coast leo imemhukumu Simone Gbagbo aliyekuwa mke wa Rais wa nchi hiyo Laurent Gbagbo, kifungo cha miaka 20 gerezani.
 
Laurent Gbagbo akiwa na mkewe Simone Gbagbo baada ya kukamatwa Aprili 11, 2011.
Simone amehukumiwa kifungo hicho baada ya kukutwa na hatia ya kushiriki katika vurugu zilizotokea baada ya uchaguzi nchini humo mwaka 2010 - 2011 ambapo watu takribani 3,000 wlipoteza maisha.

Simone Gbagbo mwenye umri wa miaka 65 alikamatwa Aprili 11, 2011 pamoja na mumewe, aliyekuwa rais wa nchi hiyo ambaye anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu katika mahakama ya uhalifu mjini The Hague, Uholanzi.
Machafuko hayo yalitokea nchini Ivory Coast mwaka 2010 baada ya Laurent Gbagbo kukataa kuachia madaraka kwa mpinzani wake Alassane Ouattara aliyekuwa ametangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi wa rais.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...