Thursday, March 12, 2015

MASTAA HAWA WAMECHEZEA MIOYO YAO!

Wema Sepetu na Diamond.
MAPENZI ni kizunguzungu! Msemo huu umetimia kwa baadhi ya mastaa waliokuwa na uhusiano ambao ulivuma kwenye vyombo mbalimbali vya habari na hawakukauka midomoni mwa watu.
Katika uhusiano huo wa kimapenzi wapo ambao walikuwa wanafurahishwa na ‘kapo’ za mastaa hao kutokana na jinsi walivyokuwa wakiendana lakini waliishia kuanguka kwenye dhambi ya uzinzi na wengine kuzaa kisha kuachana solemba, wakiridhia kuchezeana mioyo yao huku kiu ikiwa bado kwa mashabiki wao kuwaona wakiwa pamoja.

Katika makala haya tunakuletea listi ya mastaa ambao walikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi ambapo waliishia kuonjeshana na kumwagana bila kutimiza malengo ya kufikia hatua ya kufunga ndoa.
WEMA & DIAMOND
Wema Sepetu na Mbongo-Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ walikuwa ni wapenzi kwa muda mrefu ambapo kapo yao ilikuwa ikiwafurahisha mashabiki wao wengi lakini waliishia kuchezeana na kumwagana. Kipindi cha uhusiano wao walijinadi kwenye vyombo vya habari kwamba watafunga ndoa.

Hadi leo mashabiki wengi wanaitamani kapo hiyo irudi lakini ndiyo imeshatokea kwani kwa sasa Diamond ana mpenzi mwingine ambaye ni Mganda, Zarinah Hassan ‘Zari’ anayedaiwa kuwa ni mjamzito huku Wema naye akiwa na maisha yake mengine.
Rose Ndauka na Malick Bandawe.
ROSE NDAUKA & MALICK BANDAWE
Rose anayefanya vizuri katika gemu la filamu Bongo na Malick walimwagana wakiwa katika hatua za mwisho za kuingia kwenye ndoa kwani ndiyo vikao vya harusi vilikuwa vianze.
Rose aliishia kuzalishwa na Malick na uchumba wao ukavunjika kwa kile kilichodaiwa ni kukosekana kwa uaminifu ambapo hadi sasa kila mmoja ana maisha yake.Mashabiki waliipenda kapo hiyo kwani Rose baada ya kuwa na Malick alibadilika hivyo mabadiliko yake yakawa yanawavutia baadhi ya watu.
RAY & MAINDA
Uhusiano wa mastaa hao wa filamu za Kibongo ulitikisa enzi hizo na ulidumu kwa muda mrefu japokuwa walikuwa wakifanya siri lakini baada ya kuachana Mainda aliweka wazi jinsi yeye na Ray walivyochezeana na kuachana.

Mainda na Ray waliachana baada ya Ray kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii mwenzake, Chuchu Hans ambapo baada ya kumwagana kwa wawili hao mashabiki wengi walilalamika na hadi leo wanatamani Mainda na Ray warudiane kwani walikuwa wanaendana tofauti na Chuchu Hans lakini ndiyo hivyo wameachana njia panda.
AMANDA & BWANA MISOSI.
AMANDA & BWANA MISOSI
Amanda aliingia kwenye mahaba mazito na Bwana Misosi ambapo alimtambulisha hadi kwa ndugu huku wakitangaza kwamba lazima waoane lakini mbio zao ziligonga mwamba baada ya kumwagana.
Kwa sasa wawili hao wamebaki stori tu japokuwa hakuna ambaye yupo tayari kufunguka sababu za kuachana kwao lakini kila mmoja anaendelea na maisha yake mengine.

AUNTY LULU & BOND
Uhusiano wa mastaa hao ulidumu kwa muda mrefu japokuwa ulikuwa ni wa kupigana mangumi kila wakati lakini walikuwa wakipendana. Wawili hao walikuja kumwagana na kila mmoja kuchukua hamsini zake.

Kwa sasa Bond anadaiwa kuwa kwenye uhusiano na mwigizaji mwenzake, Wastara Juma huku Aunty Lulu naye akiwa na uhusiano mwingine.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...