Sunday, March 8, 2015

IVO MAPUNDA AGEUKA DJIBRIL CISSE WA BONGO


Unamkumbuka straika wa Kifaransa na klabu za Liverpool, Marseille, QPR, Sunderland na nyinginezo nyingi Djibril Cisse? Kwa taarifa yako nguli huyu hakuwa mkali wa kutishia dunia kisoka, lakini jambo lililomtambulisha zaidi duniani ni kuwa kinara wa staili za kunyoa.
Cisse alikuwa hatari sana kwa mitindo ya kunyoa na jinsi alivyopakaa rangi ndevu, nyuso na kila aina kinyweleo.
Sasa na Tanzania tunaye Cisse, Ivo Mapunda, kipa wa Simba ambaye leo alikuwa kivutio cha aina yake katika mchezo dhidi ya timu yake ya zamani, Yanga.
Angalia picha zenyewe, kisha mkumbuke Cisse wa Ufaransa.
Ivo Mapunda katikati jinsi alivyotokea katika mchezo wa leo, ndevu  na nyuso zake zikiwa zimetapakaa rangi. Ni staili ya aina yake katika soka la Tanzania.

No comments:

Post a Comment

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...