Wednesday, March 11, 2015

DIAMOND AFIKISHA MASHABIKI LAKI TANO INSTAGRAM

Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya, Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz'.
Muonekano wa akaunti yake Instagram.
MSANII mahiri wa muziki wa kizazi kipya, Naseeb Abdul 'Diamond Platinumz' amefikisha mashabiki  laki tano (500,000) kupitia akaunti yake katika mtandao wa kijamii wa Instagram.
Kupitia akaunti yake hiyo ya Intagram, Diamond aliwashukuru mashabiki wake wanaozidi kumsapoti kula kukicha kwa kuandika maneno yafuatayo: "Familia siyo tu watu ambao umezaliwa pamoja nao, ila ni pamoja na wale ambao upo nao saa 24 kwa uzuri au kwa ubaya, ambao wanakupenda au wanakuchukia. Hiyo ndiyo familia.
Akiwa katika pozi.
Nawapongeza sana wanafamilia wangu wa Instagram kwa kufikia nusu milioni" Aliandika staa huyo.
Kwa sasa staa huyo ndiye msanii mwenye mashabiki wengi katika mtandao Instagram.

POSTED TITLE

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...